Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka amchumbia mrembo Tolami

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kwamba staa huyo wa Arsenal alimvika pete mrembo Tolami katika tukio lililofanyika kwenye mtoko mmoja wa kimahaba katika hoteli moja ya huko London.

LONDON, ENGLAND: BUKAYO Saka amethibitisha kumchumbia mpenzi wake wa siku nyingi, mrembo Tolami Benson baada ya kuposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kinachoelezwa ni kwamba staa huyo wa Arsenal alimvika pete mrembo Tolami katika tukio lililofanyika kwenye mtoko mmoja wa kimahaba katika hoteli moja ya huko London.

Na sasa, Saka na mrembo Tolami, ambao umri wao unafanana, miaka 24, sasa waliamua kuwaambia mashabiki wao furaha hiyo kwa kuposti picha zao Instagram.

Posti hiyo iliandikwa maelezo ya “17.11.25,” ikielezea tarehe ambayo Saka alipiga goti kuomba ridhaa ya kumchumbia mrembo Tolami.

Wapendanao hao wamekuwa pamoja tangu mwaka 2020. Saka na Tolami wamekuwa wakiufanya uhusiano wao kuwa wa siri, lakini ilionekana kuna kitu baina yao wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2022 zilizofanyika Qatari.

Mrembo Tolami alikwenda kumsapoti Saka kwenye michuano ya Euro 2024, alipoonekana amevaa jaketi lenye namba 87, ikiwa ni namba ya kwanza kabisa aliyokuwa akivaa Saka wakati alipopandishwa kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal.

Wachezaji wenzake kwenye kikosi cha Arsenal  wakiwamo William Saliba, Gabriel Magalhaes na Eberechi Eze wote walikomenti kwa meseji za emoji. Posti hiyo iliwapendeza watu 280,000.