Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saa ya Messi ya sh2.3 bilioni yazua gumzo

MESSI Pict

Muktasari:

Nyota huyo wa Inter Miami alionekana na saa hiyo adimu sana Jumamosi usiku wakati timu yake ikitoka sare ya 0-0 dhidi ya FC Cincinnati.

FLORIDA, MAREKANI: STAA wa Inter Miami na Argentina, Lionel Messi ameonekana akiwa amevaa saa ya kifahari ya rangi ya waridi inayojulikana kama Rolex Daytona “Barbie”, yenye thamani ya takribani Pauni 700,000 (zaidi ya Sh2.3 bilioni).

Nyota huyo wa Inter Miami alionekana na saa hiyo adimu sana Jumamosi usiku wakati timu yake ikitoka sare ya 0-0 dhidi ya FC Cincinnati.

Messi, mwenye umri wa miaka 38, hakuwa uwanjani kwani alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa kucheza mechi moja.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or alikaa jukwaani pamoja na mtoto wake Thiago (12), akiwa amevalia shati jeupe lenye mvuto na kaptura ya beige  lakini kilichoteka shoo kilikuwa ni saa yake ya ajabu ya Rolex Barbie.

Saa hiyo ya kipekee imetengenezwa kwa madini ya pink sapphire yanayolingana na rangi ya jezi ya nyumbani ya Inter Miami, na pia ina dhahabu ya kiwango cha juu cha karati 18.

Ripoti zinaeleza kuwa ni saa 10 tu kama hiyo ndizo zimetengenezwa na Rolex na hazipatikani madukani, wala hazijawahi kutangazwa rasmi na kampuni hiyo.

Badala yake, Rolex inadaiwa kuwasiliana binafsi na wateja wake wa kipekee waliotathminiwa kuwa na kuzitengeneza kwa ajili yao.

Inaaminika kwamba watu mashuhuri wenye saa hizo wamelipia karibu Pauni 310,000 (takribani Sh1 bilioni), lakini ikiwa mojawapo ya saa hizo itauzwa tena sokoni, thamani yake inaweza kufikia au kuzidi Pauni 700,000.

Mtu pekee aliyewahi kuonekana na saa hiyo kabla ya Messi ni muigizaji Mark Wahlberg.

Baada ya kushuhudia mechi ya Inter Miami kwenye Uwanja wa Chase mjini Fort Lauderdale, Messi na familia yake walienda kuhudhuria tamasha la Coldplay.

Aliandamana na mkewe mrembo Antonela Roccuzzo pamoja na watoto wao watatu.

Messi pia aliingia kwenye vichwa vya habari alipokuwa kwenye tamasha hilo baada ya yeye na Antonela kuonyeshwa kwenye skrini wakikumbatiana.