Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rundo la wachezaji lamchosha Pep Guardiola

RUNDO Pict

Muktasari:

  • Pep ambaye alishuhudia staa wake Erling Haaland akifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wolves, ana wasiwasi wafanyakazi wengine kuanzia kwa benchi la ufundi na wale wa klabu watashindwa kudumisha mshikamano wa wachezaji bila idadi kupungua.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola alikiri idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi chake siyo salama kwa morali ya timu na kudai baadhi ya wachezaji wataondoka kabla ya dirisha hili kufungwa.

Man City kwa sasa ina wachezaji zaidi ya 30 kwenye kikosi chao na walau  sita wanatarajiwa kuondoka katika wiki zijazo.

Pep ambaye alishuhudia staa wake Erling Haaland akifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Wolves, ana wasiwasi wafanyakazi wengine kuanzia kwa benchi la ufundi na wale wa klabu watashindwa kudumisha mshikamano wa wachezaji bila idadi kupungua.

“Tuna watu wengi sana,” alisema Guardiola. “Leo hatukuwa na Ederson, Rodri, Phil Foden, Mateo Kovacic, Savinho na Josko Gvardiol.

“Kwenye benchi tulikuwa na Nathan Ake na Ilkay Gundogan. Napenda kikosi kirefu ili kushindana katika mashindano yote lakini sitaki kuwaacha wachezaji nyumbani.

“Hii si nzuri. Huwezi kuunda hali nzuri au hali ya kushindana. Klabu inajua hili tangu msimu uliopita lakini hali ilivyo, ndicho kinachoendelea.”

Ederson ambaye aliachwa nje ya kikosi na anahusishwa na Galatasaray, huku Tottenham inayohitaji huduma ya winga wa Brazil, Savinho.

Vile vile, Nottingham Forest imeonyesha nia ya kumsajili Rico Lewis na tayari wamefanya uhamisho wa Pauni 30 milioni kumsajili James McAtee kutoka kwa matajiri hao wa Jiji la Manchester.

Kalvin Phillips na Claudio Echeverri pia wanauzwa na wanadaiwa wataondoka  dirisha la usajili kufungwa.

“Katikati ya wiki mbili zijazo, viongozi watazungumza na wachezaji na mawakala ili kupata suluhisho,” Pep aliongeza.