Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rooney aanika mkeka wake EPL

ROONEY Pict

Muktasari:

  • Gwiji huyo wa England na Manchester United kwa sasa ni mchambuzi wa soka na analipwa mkwanja mrefu kwa msimu, Pauni 800,000.

LONDON, ENGLAND: WAYNE Rooney ametoa utabiri wa mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, huku akiwataja Liverpool watabeba taji hilo msimu huu wa 2025/26.

Gwiji huyo wa England na Manchester United kwa sasa ni mchambuzi wa soka na analipwa mkwanja mrefu kwa msimu, Pauni 800,000.

Hata hivyo, kwenye utabiri wake Rooney ameiondoa kabisa timu yake ya zamani ya Man United kwenye Top Four.

Rooney hakutazama upinzani wa Liverpool kwa kutabiri ni wao ndiyo watakaomaliza nafasi ya kwanza, huku Arsenal ikishika namba mbili, Manchester City ya tatu na Chelsea itakamilisha kwenye namba nne.

Lakini, kikosi cha Man United chini ya kocha Ruben Amorim kwa mujibu wa utabiri wa Rooney itakamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kwa sababu itamaliza kwenye nafasi ya tano, nafasi 10 juu ya ilivyomaliza msimu uliopita.

Rooney alisema: “Nadhani watahitaji usajili wa mchezaji mmoja au wawili zaidi. Ninachodhani, Amorim atakwenda kufanya vizuri na Man United itamaliza kwenye Top Five.”

Kwenye ishu ya Kiatu cha Dhahabu, Rooney alitabiri Mohamed Salah ndiye atakayekuwa kinara wa mabao kwenye ligi huku akisifia usajili wa Jeremie Frimpong huko Liverpool.