Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Red Bull Salzburg yafikiria kumsajili Sadio Mane

Muktasari:

  • Mane ambaye alijiunga na  Al-Nassr katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, akisaidia kufuzu Ligi ya Mabingwa barani Asia msimu ujao na kufunga mabao 13 katika Ligi Kuu Saudi Arabia amekuwa akiripotiwa kwamba anataka kurudi Ulaya kwa ajili ya kupata ushindani zaidi.

WAKALA wa Sadio Mane Bjorn Bezemer amesisitiza kuwa mchezaji wake  huyo ana furaha kuendelea kucheza Al Nassr na hakuna timu yoyote kutoka Ulaya iliyofanya naye mazungumzo katika dirisha hili licha tetesi kudai kwamba anaweza kujiunga na Red Bull Salzburg ya Austria.

Mane ambaye alijiunga na  Al-Nassr katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, akisaidia kufuzu Ligi ya Mabingwa barani Asia msimu ujao na kufunga mabao 13 katika Ligi Kuu Saudi Arabia amekuwa akiripotiwa kwamba anataka kurudi Ulaya kwa ajili ya kupata ushindani zaidi.

Ripoti nchini Austria zilieleza ma huenda akarejea Salzburg kujiunga na kocha wake wa zamani wa Liverpool Pep Lijnders  ambaye ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Staa huyu wa kimataifa wa Senegal aliwahi kuichezea Sulzburg kuanzia mwaka 2012 hadi 2014 alipojiunga nayo akitokea Metz na baada ya hapo ndio akatua Southampton.

"Sijakutana na klabu yoyote kujadili kuhusu Mane, kwa sasa yupo katika maandalizi ya kuitumikia  Al Nassr katika msimu mpya  na wala hana  kabisa mpango wa kuondoka, pia timu bado inamhitaji na inafurahia uwepo wake."

Akiwa na Salzburg, Mane alifunga mabao 45 katika mechi 87 ndani ya misimu hiyo miwili pia alichukua taji la Ligi Kuu Austria mwaka 2014.

Mara kadhaa amewahi kuizungumzia timu na Jiji la Salzburg akisema:"Nalipenda jiji na timu, kama ilivyokuwa hapo mwanzo na sasa pia iko hivyo.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 32 bado ana mkataba wa kuitumikia Al Nassr hadi mwaka 2026.