Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Real Madrid yaachana na mpango wa  Rodri

Muktasari:

  • Taarifa zinaeleza bei hiyo kubwa, sambamba na umri wa mchezaji huyo mwenye  miaka 29, ni miongoni mwa sababu zilizowafanya vigogo hao wa Hispania kuamua kusitisha kabisa mpango wa kumsajili.

REAL MADRID imeonekana kupunguza kabisa nia yake ya kumsajili kiungo wa Manchester City, Rodri, baada ya kubaini dili hilo linaweza kuwagharimu si chini ya Euro 60 milioni dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Taarifa zinaeleza bei hiyo kubwa, sambamba na umri wa mchezaji huyo mwenye  miaka 29, ni miongoni mwa sababu zilizowafanya vigogo hao wa Hispania kuamua kusitisha kabisa mpango wa kumsajili.

Hata hivyo, Rodri ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Man City, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na hadi bado hajasaini.

Taarifa za ndani zinadai kuna uwezekano mkubwa Madrid ikarudi mezani mwakani ifikapo Januari na atakuwa amebakisha miezi sita kabla ya mkataba kumalizika, hivyo inaweza kumpata kwa bei rahisi wakati huo.

Kwa sasa, Madrid inataka kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wachezaji ambao watakuwa na umri mdogo tu kwa ajili ya kuwatumia kwa muda mrefu lakini kwa staa kama Rodri inaona ni hasara kutoa kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika.


Dele Alli

ALIYEKUWA kiungo wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya England, Dele Alli, mwenye umri wa miaka 29, amerejea kufanya mazoezi na Spurs ikiwa ni katika maandalizi ya kujiandaa kurudi katika soka la kiushindani. Dele amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuachana na Como ya Italia Septemba mwaka jana ambayo ilivunja mkataba. Hadi sasa hakuna timu iliyohusishwa naye ingawa inaaminika kuna uwezekano mkubwa akapata timu ifikapo mwisho wa msimu.


Khephren Thuram

ARSENAL, Liverpool na Manchester United zinatajwa kuingia kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Khephren Thuram, mwenye umri wa miaka 24. Taarifa zinaeleza vigogo hao wa Ligi Kuu England wanaangalia uwezekano wa kumsajili staa huyo, ambaye ameonyesha kiwango bora katika Serie A kwa muda mrefu. Juventus bado haijaweka wazi msimamo wao kuhusu mustakabali wa Thuram, lakini baada ya timu hizo kuonyesha nia ya kumsajili kuna asilimia kubwa ikakubali kumuuza.


Antoine Griezmann

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann, 34, yupo njiapanda juu ya mustakabali wake akiwa bado hajafanya uamuzi ikiwa ajiunge na  klabu ya Marekani ya Orlando City au asalie Atletico. Taarifa zinaeleza Griezmann anafikiria kwanza kwa kina chaguo kabla ya kufanya uamuzi wa wapi aende dirisha lijalo. Mkataba wa sasa wa Griezmann unatarajiwa kumalizika mwaka.


Michael Olise

TARIFA zinaeleza Liverpool imebadilisha gia angani na sasa inataka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Yan Diomande, baada ya kuona kuwa haitoweza kufanikisha dili la kumsajili kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise, kutoka Bayern Munich. Bayern Munich haitaki kumuuza Olise na sasa ipo katika mazungumzo ya kumuongeza mkataba  mpya utakaomwezesha kuendelea kusalia katika viunga hivyo wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Michael Kayode

MANCHESTER United na Newcastle United zimeingia katika orodha ya  klabu zinazomfuatilia beki wa kulia wa Brentford na timu ya taifa ya vijana ya Italia, Michael Kayode, 21. Kayode ambaye alijiunga na Brentford mwaka jana amekuwa bora sana katika EPL kwa msimu huu na hiyo imefanya timu nyingi kummezea mate. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, Kayonde mwenyewe hana presha licha ya kuhusishwa na vigogo hao. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Paulo Dybala

ROMA imewaambia nyota wao Paulo Dybala, 32, na Lorenzo Pellegrini, 29, watatakiwa kukubali kupunguziwa mishahara ikiwa wanahitaji  kuendelea kusalia katika timu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa, wachezaji hao watalazimika kupunguza mishahara yao baada ya mikataba yao inayomalizika mwisho wa msimu kuisha. Uongozi wa Roma unapambana kwa ajili ya kujikwamua katika hali mbaya ya kiuchumi ambayo klabu inapitia.


Lucas Bergvall

TOTTENHAM Hotspur bado haina mpango wa kukubaliana na maombi ya Aston Villa na Chelsea zinazohitaji kumsajili kiungo wao wa kimataifa wa Sweden, Lucas Bergvall, 20, mwisho wa msimu.

Bergvall anaonekana kuwa sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya Spurs, baada ya kuonyesha kiwango bora tangu ajiunge na klabu hiyo. Viongozi wa Spurs wanataka kusubiri walau kwa msimu mmoja au miwili kabla ya kumuuza wakiamini wakati huo watapata pesa nyingi zaidi tofauti na ilivyo saa. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2031.