Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford mambo freshi La Liga

RASH Pict

Muktasari:

  • Hii ni baada ya kipa wa miamba hiyo ya Catalonia, kumrudishia kitambaa cha unahodha kipa wao, Marc-Andre ter Stegen, ambaye alisaini pia ripoti ya matibabu.

MANCHESTER, ENGLAND: STAA wa Manchester United anayecheza kwa mkopo Barcelona, Marcus Rashford ni moja ya majina saba ambayo huenbda yakaingia katika orodha ya nyota watakaokipiga La Liga msimu ujao.

Hii ni baada ya kipa wa miamba hiyo ya Catalonia, kumrudishia kitambaa cha unahodha kipa wao, Marc-Andre ter Stegen, ambaye alisaini pia ripoti ya matibabu.

Awali, mabosi wa Barcelona walitaka kufanikisha uwezekano wa nyota hao kuandikishwa, kwa kipa huyo kusaini ripoti hiyo ya kutokuwepo kikosini kwa muda kutokana na kuuguza majeraha.

Kipa huyo, 33, alishindwa kufanya hivyo tangu alipofanyiwa upasuaji wa mgongo mwezi uliopita, akiiambia klabu atakosa mechi kwa miezi mitatu tu, hivyo hawezi kusaini karatasi hizo.

Baada ya nyota huyo kugoma ndipo akavuliwa unahodha kabla ya jana kufanya kubadili maamuzi na kusaini.

Kwa hatua hiyo sasa, kuna uwezekano mkubwa Rashford, akawa miongoni mwa watakaoingia kikosini na kucheza mchezo wa kwanza wa La Liga.

Winga huyo wa kimataifa wa England, 27, ameonyesha kiwango bora katika maandalizi ya msimu na alifunga bao dhidi ya timu ya Korea Kusini, Daegu.

Mbali na Rashford, mchezaji mwingine mpya Roony Bardghji pia a huenda akawepo kikosini.

Mapema katika dirisha hili, Barcelona ilisajili kipa Joan Garcia kutoka kwa wapinzani wao, Espanyol, kama mbadala wa Ter Stegen anayeuguza majeraha.

Wingine ni kipa Wojciech Szczesny, achezaji wachanga kama Marc Bernal, Gerard Martin na Hector Fort.

Mchezaji wa zamani wa Southampton, Oriol Romeu, pia amekuwa akisubiri kuingia kikosini kukipiga mchezo wake wa kwanza wa La Liga..

Kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita, Barcelona inajitahidi kufuata kanuni za kifedha za LaLiga na kuhakikisha wachezaji wao wote wanaandikishwa.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Hansi Flick itaanza kampeni yao dhidi ya RCD Mallorca Agosti, 16 ya wiki hii.