Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford mambo bado La Liga

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Fowadi huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Manchester United.

BARCELONA, HISPANIA: MARCUS Rashford amefunga bao lake la kwanza Barcelona huku kikosi hicho kikipambana kwa nguvu zote kuhakikisha inamwandikisha Mwingereza huyo ili kuwa na kibali cha kucheza kwenye La Liga.

Fowadi huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Manchester United.

Na bao lake la kwanza kwenye kikosi cha Barca alifunga kwenye ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Daegu FC ya Korea Kusini, Jumatatu. Lamine Yamal alionyesha kiwango bora kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi kadhaa.

Rashford alishika mguu wa kushoto wa Lamine wakati anaingia na hilo lilikuwa na baraka kwake, alipofunga dakika ya 65.

Hata hivyo, licha ya kucheza mechi ya tatu ya kirafiki akiwa na Barcelona, Rashford bado hajaorodheshwa kucheza kwenye La Liga.

Barca inapambana kufikia vigezo vya mshahara kwenye La Liga jambo linalowaweka kwenye wakati mgumu wa kuandikisha wachezaji wapya. Sakata kama hilo liliwakabili msimu uliopita, wakati mchezaji Dani Olmo, aliyelazimika kusubiri kwa muda kucheza mechi yake ya kwanza kwenye ligi baada ya kusajiliwa majira ya kiangazi mwaka 2024.

Miamba hiyo ilipewa kibali cha muda na La Liga kuwaandikisha wachezaji Olmo na Victor mwaka jana.

Sambamba na Rashford, Barcelona inakabiliwa na wakati mgumu pia wa kuwaandikisha wachezaji wengine wapya Joan Garcia na Roony Bardghji, pamoja na kipa Wojciech Szczesny na beki Gerard Martin.

Lakini, zikiwa zimebakia wiki mbili kabla ya mechi ya kwanza ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Mallorca, Rashford amekuwa hana wasiwasi, akiamini mabosi wa Barcelona watambana kwa nguvu zote kufanya jambo hilo kutiki.

Rais wa Barcelona, Joan Laporta alisema: “Tumemsajili huyu mchezaji kwasababu ametaka kuja Barcelona. Ana kasi, nguvu na kila kitu kinachohitajika ili kusajiliwa na Barca.”