Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford kusubiri kwanza Barcelona

Muktasari:

  • Rashford, 27, amejiunga na Barca kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima akitokea Manchester United.

BARCELONA, HISPANIA: BARCELONA imefuta mechi ya kwanza ya kirafiki kwenye pre-season jambo litakalomchelewesha Marcus Rashford kuitumikia timu yake mpya mapema.

Rashford, 27, amejiunga na Barca kwa mkataba wa mkopo wa msimu mzima akitokea Manchester United.

Mabingwa hao wa La Liga watakuwa na ruhusa ya kumsajili jumla mkali huyo kwa dau la Pauni 26 milioni wakati wa dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Kwa sasa, Rashford akili yake ipo kwenye kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Hansi Flick huko Camp Nou.

Jumapili, Barca ilitarajia kumenyana na Vissel Kobe ya Japan kwenye mechi ya kirafiki, lakini mechi hiyo haipo tena baada ya viongozi wa Barcelona kufichua kwamba promota amekiuka vipengele vya mkataba.

Kuahirishwa kwa mechi hiyo kunakwenda sambamba pia na tangazo la kuchelewa kuutumia uwanja wao wa Camp Nou baada ya kufanyiwa maboresho.

Awali, mapema mwezi huu ilitangaza Barca itakipiga na Como ya Italia, Jumapili ya Agosti 10, ambapo itakuwa mechi ya kwanza baada ya kurejea kwenye uwanja huo uliokuwa ukifanyiwa maboresho kwa miaka miwili. Lakini, sasa jambo hilo halitatokea hadi hapo uwanja utakapokamilika kabisa.

Barcelona sasa inasikilizia hatima ya mechi nyingine za kirafiki kwenye pre-season zitakazofanyika Korea Kusini, ambapo watakipiga na FC Seoul (Julai 31) na Daegu FC (Agosti 4) baada ya promota kukidhi matakwa yao.

Kwa sasa kikosi hicho kinafanya mazoezi Catalunya, ambapo Rashford aliungana na wachezaji wenzake kwenye kipindi cha mazoezi ya Jumatano.

Wakati huo huo, Rashford, 27 amerudiana na mchumba wake, mrembo Lucia Loi, ambaye alimchumbia Juni 2022 kwa kumvita pete ya Pauni 250,000.

Lakini, uchumba huo ulikufa Juni 2023 kabla ya staa huyo wa England kuangukia kwenye penzi la mrembo Grace Jackson, ambapo waliachana Desema 2023.

Na sasa Rashford amerudi kwa Lucia, kipenzi cha roho yake tangu utotoni na walikuwa wote pamoja wakati anatambulishwa Barcelona.