Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford aweka wazi ishu ya Barcelona

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa Manchester United, ambaye amewekwa pembeni na Ruben Amorim, alisema anatamani kucheza pamoja na nyota Lamine Yamal.

BARCELONA, HISPANIA: STAA wa Manchester United, Marcus Rashford ameweka wazi anataka kujiunga na Barcelona dirisha hili ikiwa itapatikana nafasi hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Manchester United, ambaye amewekwa pembeni na Ruben Amorim, alisema anatamani kucheza pamoja na nyota Lamine Yamal.

Rashford anadai yuko tayari hata kubadilika kutoka nafasi yake ya kawaida ya winga hadi kuwa mshambuliaji wa kati namba 9 ili kufanikisha uhamisho huo.

Akizungumza na kituo cha YouTube cha Kihispania XBuyer akiwa Marbella, Rashford aliulizwa kama angependa kucheza na Yamal siku moja.

Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alicheza Aston Villa kwa mkopo alijibu: "Ndiyo, bila shaka. Kila mtu duniani anataka kucheza na timu bora. Kwa hiyo tumuombe Mungu, tutaona..."

Kuhusu kubadilika kutoka winga hadi mshambuliaji wa kati, Rashford aliongeza: "Kwangu mimi kadri ninavyoendelea kuwa mkubwa, nafasi ya namba 9 inakuwa ya kawaida zaidi, naelewa zaidi nikicheza hapo."

Rashford pia alimsifia Yamal na hata kumtabiria kushinda Ballon d’Or.

"Yamal anakua... ni vigumu kuelezea anachofanya kwa sababu hapaswi kuwa anafanya hayo kwa sasa akiwa na umri wa miaka 16, 17. Anacheza katika kiwango cha juu kabisa, sidhani kama tumeona kitu kama hiki. Kuwa na akili kama yake ni kipaji. Si jambo la kawaida kufanya anachofanya na anaendelea kuimarika."

Rashford kwa sasa yuko likizo Hispania ambako anafanya mazoezi kujiandaa na msimu ujao licha ya kwamba haijajulikana ni timu gani ataichezea.

"Hispania ni kuzuri kwanza si mbali sana na nyumbani, familia yangu inaweza kuja kwa siku chache, ni sehemu nzuri na hali ya hewa nzuri."