Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford atafuta nafasi Barcelona

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Staa huyo wa Manchester United amewekwa kando na Kocha Ruben Amorim, sasa amefichua ndoto zake za kwenda kucheza timu moja na supastaa wa Barcelona, Lamine Yamal kwenye mahojiano yake akiwa kwenye mapumziko.

BARCELONA, HISPANIA: STAA, Marcus Rashford amesema anataka kwenda kujiunga na Barcelona ikiwa ni ujumbe wa kijanja anaotuma kwa Wahispaniola hao ‘njooni mnichukue’.

Staa huyo wa Manchester United amewekwa kando na Kocha Ruben Amorim, sasa amefichua ndoto zake za kwenda kucheza timu moja na supastaa wa Barcelona, Lamine Yamal kwenye mahojiano yake akiwa kwenye mapumziko.

Rashford yupo tayari hata kubadilisha nafasi yake anayocheza kwenye wingi ili akatumike kwenye Namba 9 ili tu jambo hilo litaokee.

Akizungumza na Chaneli ya Youtube ya XBuyer huko Marbella, Rashford aliulizwa kama kama anataka kwenda kucheza timu moja na Yamal siku moja.

Winga huyo Mwingereza, ambaye aliitumikia Aston Villa kwa mkopo msimu uliopita: “Ndio, hakika. Kila mtu duniani anataka kucheza na waliobora. Hivyo, natumai, ngoja tuone...”

Kuhama kutoka kwenye winga hadi mshambuliaji wa kati, Rashford aliongeza: “Kwangu upande wangu, kwa kadri ninavyokuwa mkubwa, Namba 9 inaonekana kuwa nzuri zaidi kwangu, nitatulia hapo. Vitu kama kucheza mbele ya goli ni vitu rahisi kwangu, nitapokuwa mbele ya goli, siku zote nimekuwa hatari.”

Rashford aliendelea kuimba nyimbo za kumpamba Yamal na kufikia hatua ya kuamini kwamba atakwenda kushinda tuzo ya Ballon d’Or, aliposema: “(Yamal) atafika… ni ngumu kueleza kwa maneno kutokana na kile anachofanya hasa ukizingatia umri wake wa miaka 16, 17. Anacheza kwenye kiwango kikubwa, sidhani kama tumeshawahi kuona kitu kama hiki. Kuhusu Ballon d’Or, ukitazama namba zake anakwenda kushinda, lakini kuna Ousmane Dembele, ana taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya…”

Rashford kwa sasa yupo mapumzikoni Hispania na amekuwa akifanya mazoezi kivyake ili kujiandaa na pre-season. Staa huyo alikiri kupendezwa na nchi ya Hispania aliposema: “Hispania ni pazuri, sio mbali na nyumbani. Kama nitakuwa hapa kwa muda mrefu, familia yangu itaweza kuja siku chache, ni mahali pazuri na hali ya hewa ni nzuri.”