Ramani ya Xabi Alonso akitua Chelsea
Muktasari:
- Kuna jambo linahitaji kubadilika ndani ya Chelsea, na siyo tu kocha tu, kwani licha ya Liam Rosenior kuwa tayari nje ya mlango, lakini kila mtu anajua matatizo ni zaidi ya kocha.
LONDON, ENGLAND: CHELSEA imepitia katika kipindi kigumu ndani ya kipindi kifupi, ambapo imeachana na makocha wawili ndani ya miezi minne ya mwaka 2026 na sasa iko chini ya kocha wa muda, Calum McFarlane na hivyo, kwa mabosi watakuwa wanapambana mezani na majina kadhaa ya makocha wasio na ajira na walionazo ili wakakinoe kikosi hicho.
Hata hivyo, licha ya kuwa na majina mengi, lakini lile la Xabi Aloso limeendelea kugonga vichwa vya habari likipewa nafasi kubwa ya kutua katika kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu, na hapa ni jinsi Chelsea inavyoweza kupanga kikosi chini ya Alonso na uuzaji wa nyota muhimu sambamba na mfumo mpya unaweza kushangaza.
Kuna jambo linahitaji kubadilika ndani ya Chelsea, na siyo tu kocha tu, kwani licha ya Liam Rosenior kuwa tayari nje ya mlango, lakini kila mtu anajua matatizo ni zaidi ya kocha.
Chelsea hawana uwiano katika maeneo yote mawili ya uwanja na wana mastaa wa kiungo wenye thamani ya Pauni 200 milioni+ ambao bado wanahitaji mtu mwingine pembeni yao ili kiwe na ufanisi.
Hivyo yeyote atakayekuwa kocha mkuu ajaye hana uwezekano wa kufanya kama Thomas Tuchel kuibadilisha timu hiyo ya vijana wenye matumaini kuwa na ushindani katika Ligi ya Mabingwa.
Achana na maelezo yote hapo juu, jina la Alonso, kocha wa zamani wa Real Madrid na Bayer Leverkusen linaweza kuwa na suluhisho. Akiwa na uzoefu, mataji aliyoshinda akiwa mchezaji na kocha pamoja na uelewa wa Ligi Kuu England kutokana na muda wake aliocheza Liverpool, Mhispania huyo anakidhi vigezo vingi.
Lakini, kama wengine wote, Alonso atahitaji nyongeza katika kikosi chake ili aweze kufanya kazi yake kwa mafanikio. Hivyo hapa ni jinsi anavyoweza kupanga kikosi baada ya dirisha la usajili la majira ya joto.
KIKOSI CHA KWANZA MFUMO WA 3-4-3
Uamuzi mkubwa wa Alonso akiwa Leverkusen ulikuwa kubadili mfumo wa mabeki watatu, na ulifanya kazi kwa mafanikio makubwa. Alikuwa na wing-back Alejandro Grimaldo na Jeremie Frimpong wakishambulia kwa kasi, huku msingi ukiimarishwa na uzoefu wa Granit Xhaka. Kama akichagua mbinu hiyo Chelsea, mabadiliko makubwa yanaweza kuwa muhimu.
Kwa kuzingatia idadi ya mabeki wanaoweza kuondoka, uimarishaji mkubwa wa kikosi unahitajika, na Alessandro Bastoni wa Inter Milan ni miongoni mwa mabeki bora zaidi wa kati anaoweza kuwachukua ili kumsaidia.
Alonso amezoea mfumo wa mabeki watatu na Ousmane Diomande wa Sporting anaweza kuungana na Bastoni. Nyuma yao, kipa Mike Penders mwenye umri wa miaka 20 anayecheza kwa mkopo Strasbourg.
Ili kulinda safu ya ulinzi, Moises Caicedo anabaki katika nafasi yake lakini Enzo Fernandez anaondoka akihusishwa mara nyingi na Real Madrid na, ili kusaidia kupunguza matatizo ya kifedha, Chelsea wanamuuza na kununua mbadala kwa gharama kubwa ambapo Amadou Onana wa Aston Villa anasimama pale juu.
Akiwa ameanza kujulikana kama wing-back, Reece James ni chaguo bora upande wa kulia, ingawa changamoto za majeraha ni tatizo.
KIKOSI CHA PILI
Mtu mwenye mashaka anaweza kusema timu zote hizo hata ile ya pili isiyo na mvuto inawezekana zikampa Alonso akitakacho? Marc Cucurella hajazoea sana mfumo huu 3-4-3, lakini anaingia. Geovany Quenda anaweza kumpa ushindani katika kuipambania timu hiyo.
Katika safu ya ushambuliaji, Joao Pedro na Cole Palmer wanaendelea kushirikiana lakini nafasi ya winga wa kushoto yenye changamoto inachukuliwa na usajili mpya Anthony Gordon. Yeye ni lengo la klabu na ni mkali katika Ligi Kuu Enland, ingawa baadhi hawaridhishwi sana na ubora wake.
KIKOSI MBABALA
Kama kikosi cha kwanza ni cha gharama kubwa chenye usajili usio wa kawaida, basi hiki kinaweza kuwa cha kawaida zaidi. Kuna mabadiliko ya kipa ambapo Mike Maignan aliyepo Inter Milana anachukua nafasi ya Robert Sanchez mwaka mmoja baadaye kuliko ilivyotarajiwa na baadhi.
Na badala ya Bastoni, ni Jorrel Hato mwenye kipaji. Dogo huyo aliyezaliwa 2006 amekuwa miongoni mwa wachache walioanza kung’ara Stamford Bridge mwezi uliopita.
Badala ya kununua kiungo mwingine mkubwa, Andrey Santos anaweza kuaminiwa kupiga kazi ya Enzo Fernandez kuunda safu bora ya kujilinda.
Romeo Lavia yupo kama mbadala kama ataweza kubaki kuwa fiti katika dunia hii ya kufikirika.
Katika wing-back wanabaki walewale na ushambuliaji ni uleule, lakini Joao Pedro anashuka kuwa namba 10 anayezunguka sambamba na Nicolas Jackson anayerudi kutoka kwenye mkopo Bayern Munich.
Katika eneo hilo Jackson anacheza namba tisa na anapata nafasi ya kufufua uhusiano wake na Cole Palmer. Sanchez anabaki golini huku Penders akipata mwaka mwingine wa uzoefu huko Strasbourg.
Badala ya kufanya usajili mikoba anasimama Levi Colwill baada ya kupona majeraha akiwa na Hato, na kisha Wesley Fofana mwenye makosa mengi anakuwa benchi akisikilizia. Chelsea kweli wanahitaji mtu mwingine katika nafasi hii, lakini wamekuwa na tatizo hilo kwa muda.
Kwa kuendeleza mtindo wa BlueCo, eneo la kiungo Valentin Barco anakuja kama usajili mpya kutoka Strasbourg. Huyu ni mchezaji mwepesi, lakini hayupo karibu na ubora wa Enzo Fernandez.
Na katika ushambuliaji iwapo hatarudi Jackson na Joao Pedro anayedaiwa kwamba atauzwa Barcelona, basi straika mpya namba tisa atakuwa ni mchezaji mwingine wa zamani wa Strasbourg, nahodha wao Emmanuel Emegha.