Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSV yailaza Napoli kwa mabao 6-2

Muktasari:

  • Scott McTominay alianza kufunga na baadaye akapata bao la kufutia machozi kwa Napoli katika mechi iliyojaa matukio iliyopigwa Uwanja wa Philips, Uholanzi.

EINDHOVEN, UHOLANZI: PSV Eindhoven imepindua matokeo kwa kishindo na kuishangaza Napoli iliyomaliza ikiwa na wachezaji 10, kwa ushindi wa mabao 6-2 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezw usiku wa Oktoba 21, 2025 ukiwa ni ushindi wao wa kwanza msimu huu.

Scott McTominay alianza kufunga na baadaye akapata bao la kufutia machozi kwa Napoli katika mechi iliyojaa matukio iliyopigwa Uwanja wa Philips, Uholanzi.

Dakika saba tu baada ya bao la ufunguzi la McTominay, PSV ilikuwa imeshaongoza baada ya Ismael Saibari kufunga bao zuri kufuatia bao la kujifunga la Alessandro Buongiorno.

Dennis Man aliongeza mabao mawili kwa wenyeji, kila moja likitokea kabla na baada ya Lorenzo Lucca kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 76 kwa kumkosoa mwamuzi.

McTominay, ambaye aling’ara sana msimu wake wa kwanza akiwa na Napoli, alipunguza tofauti kwa bao dakika tano kabla ya muda wa kawaida kumalizika.

Hata hivyo, PSV ilijibu haraka kupitia Ricardo Pepi aliyerejesha pengo la mabao matatu, kabla ya Couhaib Driouech kufunga bao maridadi la mbali na kukamilisha usiku bora kwa wenyeji.

Ni kipigo cha pili mfululizo kwa kikosi cha Antonio Conte, ambacho kilipoteza nafasi ya kuongoza Serie A Jumamosi iliyopita baada ya kuchapwa na Torino.

Napoli sasa inashika nafasi ya 22 kati ya timu 36 katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, huku PSV ikipanda hadi nafasi ya 11.