Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PSG yaambiwa imlipe Mbappe Pauni 52 milioni

Muktasari:

  • Mahakama ya Marekani ilitambua kwamba PSG ilishindwa kumlipa Mbappe mshahara wake wa miezi mitatu na bonasi kati ya Aprili na Juni mwaka jana. Mbappe, ambaye kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Real Madrid alipaswa kulipwa kiasi cha Pauni 231.5 milioni kutoka kwa klabu hiyo kutokana na kukiuka vipengele kwenye mikataba yao.

PARIS, UFARANSA: SUPASTAA, Kylian Mbappe atapokea Pauni 52 milioni baada ya kushinda shauri lake mahakamani dhidi ya klabu yake ya zamani ya Paris Saint-Germain.

Mahakama ya Marekani ilitambua kwamba PSG ilishindwa kumlipa Mbappe mshahara wake wa miezi mitatu na bonasi kati ya Aprili na Juni mwaka jana. Mbappe, ambaye kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Real Madrid alipaswa kulipwa kiasi cha Pauni 231.5 milioni kutoka kwa klabu hiyo kutokana na kukiuka vipengele kwenye mikataba yao.

Staa huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 26 hakufurahishwa na namna PSG ilivyomfanyia kwenye tofauti yao ya kimkataba.

Madai hayo ya ziada yalikataliwa, lakini mahakama hiyo ilimtaka Mbappe alipwe kiwango hicho cha Pauni 52 milioni, kitu ambacho mwanasheria wake, Frederique Cassereau alisema mteja wake ametosheka na hukumu.

Mwanasheria huyo, mrembo Frederique alisema: “Hiki ndicho kitu unachokitarajia mishahara inaposhindwa kulipwa.”

Sintofahamu kubwa iliibuka baina ya Mbappe na PSG mwaka 2023 wakati mchezaji huyo alipowaambia mabosi wa timu hiyo hatakifanyia kazi kipengele cha kuongeza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huko Parc des Princes.

Mwaka mmoja kabla, Mbappe alisaini dili tamu kabisa PSG na miaka sita kabla ya hapo mabingwa hao wa Ufaransa walilipa Pauni 166 milioni kulinasa saini yake ikimng'oa kutoka AS Monaco. Na baada ya kugomea kusaini mkataba mpya PSG, Mbappe alikwenda kujiunga bure kabisa na Real Madrid mwaka 2024.

PSG ilitaka kumuuza Mbappe kwenda Al-Hilal mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Los Blancos baada ya kupokea ofa ya Pauni 259 milioni kutoka kwa Waarabu hao, lakini Mbappe aligoma kwenda kukutana na mabosi wa Al Hilal kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya maslahi binafsi. Kutokana na kukwama kwa dili hilo, PSG ilitaka ilipwe fidia ya Pauni 211 milioni, lakini mahakama iliwagomea na hivyo kutoa ushindi kwa upande wa mchezaji.

Mbappe kwa miaka yake saba aliyokuwa kwenye kikosi cha PSG alifunga mabao 256, ambayo ni rekodi katika klabu hiyo.