Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Postecoglou kumrithi Nuno Forest

POSTE Pict

Muktasari:

  • Mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis alitaka kupata kocha mpya haraka baada ya kumwondoa kazini Nuno na tayari ameshafanya uamuzi baada ya mazungumzo na aliyekuwa bosi wa Tottenham Hotspur, Postecoglou.

LONDON, ENGLAND: ANGE Postecoglou anajiandaa kuwa kocha mpya wa Nottingham Forest baada ya kufutwa kazi Nuno Espirito Santo.

Mmiliki wa Forest, Evangelos Marinakis alitaka kupata kocha mpya haraka baada ya kumwondoa kazini Nuno na tayari ameshafanya uamuzi baada ya mazungumzo na aliyekuwa bosi wa Tottenham Hotspur, Postecoglou.

Nuno aliondoshwa kazi asubuhi ya Jumanne baada ya taarifa fupi iliyotumwa kwenye tovuti ya klabu hiyo yenye maskani yake City Ground.

Kocha huyo Mreno, Nuno aliripotiwa kutibuana na bosi mwenye timu Marinakis na mkurugenzi wa soka, Edu na hivyo kuonyeshwa mlango wa kutokea wakati timu ikiwa imecheza mechi tatu tu kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England na inashika namba 10 katika msimamo.

Nuno, 51, amekuwa akiinoa Forest tangu Desemba 2023 na aliongoza timu hiyo kushika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, hivyo kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Europa League msimu huu.

Alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu Juni mwaka huu, lakini baada ya kutibuana na mabosi wake kwenye masuala ya usajili hasa baada ya ujio wa aliyekuwa bosi wa Arsenal, Edu umempeleka kwenye suala la kuachana na timu hiyo.

Postecoglou amekuwa hana kazi tangu alipotemwa na Tottenham mwishoni mwa msimu uliopita alikuwa chaguo la kwanza la tajiri Marinakis. Bosi huyo anaamini kocha huyo raia wa Australia atapeleka staili yake ya soka la kushambulia huko Forest.