Pogba kusaini Juve hadi Julai

Pogba kusaini Juve hadi Julai

PAUL Pogba atasaini mkataba wa kukipiga Juventus, itakapofika Julai, mwaka huu baada ya wawakilisha wake kufikia makubaliano na miamba hiyo kutoka Turin.
Kiungo huyo atakuwa mchezaji rasmi wa Juventus, mkataba wake utakapoisha mwisho wa mwezi huu baada ya kuagana na Manchester United.
Pogba alijiunga na Man United tangu mwaka 2016, kwa rekodi ya usajili Pauni 89 milioni, akitokea Juentus, lakini sasa kiungo huyo amerejea kwa vibibi kizee wa Turin.
Pogba atakuwa huru mwisho wa mwezi huu baada ya mkataba wake na mashetani wekundu kuisha, ikumbukwe mabosi wa klabu hiyo imeshindwa kumwongezea mkataba mwingine wa kubaki Old Trafford msimu ujao.
Kwa mujibu wa ripoti Juventus imapania kukamilisha uhamisho wa Pogba, dirisha hili la usajili, hata hivyo dili hilo lipo ukingoni kukamilika kabla ya kutambulishwa.
Pogba, 29, alionyesha nia ya kurejea Turin na kuipiga chini Manchester City iliyomtolea macho dirisha hili, awali kiungo alihusishwa na miamba ya Ufaransa, Paris Saint-Germain hata hivyo akapotezea tetesi hizo.
Pogba atakuwa akipokea mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki, uhamisho wake utakapokamilika na atasaini mkataba wa miaka mine kukipiga Turin kwa mujibu wa ripoti.
Hivi karibuni staa huyo alipondwa na mashabiki baada ya kuweka wazi, Man United ilizungua kutompa mkataba mpya, kauli hiyo aliisema kupitia makala ya maisha yake ‘Pogmentary’, iliyozinduliwa wiki iliyiopita.