Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep ajivika mabomu ishu ya Leverkusen

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Man City alikiri kwamba uamuzi wa kuanza na wachezaji tofauti  ulikuwa ni kosa kubwa lililoigharimu timu yake ambayo imejiweka katika hatari kubwa ya kucheza mechi ya hatua ya mtoano ili kufuzu 16 bora.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amejitwisha lawama zote kufuatia kichapo cha kushtua cha Manchester City dhidi ya Bayer Leverkusen baada ya kufanya mabadiliko ya wachezaji 10.

Kocha huyo wa Man City alikiri kwamba uamuzi wa kuanza na wachezaji tofauti  ulikuwa ni kosa kubwa lililoigharimu timu yake ambayo imejiweka katika hatari kubwa ya kucheza mechi ya hatua ya mtoano ili kufuzu 16 bora.

Erling Haaland, Phil Foden na Rayan Cherki walianzia benchini kabla ya kuingizwa uwanjani wakati Leverkusen ikiwa inaongoza kwa mabao mawili, lakini bado hawakuweza kubadilisha upepo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Guardiola alisema: "Nawajibika mimi kwa kilichotokea, lakini jambo zuri ni kwamba niliona wachezaji wote walivyocheza na mimi huwa napenda kila mtu ahusike. Ukiwa mchezaji wa soka na unakaa benchini kwa mechi tano, sita, saba mfululizo ni jambo gumu sana, hivyo nilitaka kuwapa wengine nafasi, lakini labda nilifanya mabadiliko mengi kupita kiasi."

Kichapo cha 2-0 kilikuwa ni cha mara ya kwanza kwa Man City kupoteza mechi ya hatua za awali nyumbani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2018.

Guardiola alidokeza kuwa ratiba ngumu ilichangia muamuzi wake huo, lakini  amesikitishwa na matokeo na kudai kuwa wachezaji wengi hawakuwa wanaonekana kujiamini.

Oscar Bobb, Rico Lewis na Rayan Ait-Nouri walitolewa wakati wa mapumziko, huku Omar Marmoush naye akitolewa baadaye.

Guardiola aliongeza: "Haiwezekani kusema hawana uwezo, nafikiri walikuwa wanafikiria sana wasije wakafanya kosa la kuiumiza timu, wakawa hawapo huru na wakashindwa kufanya mikimbio inayotakia.

Tuna michezo mingi siku zijazo. Hatuwezi kumchezesha Erling kila mechi kwa dakika 95 – tunahitaji miguu mipya, lakini nakiri kwamba nilifanya zaidi ya vile ilivyotakiwa kuwa."