Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paqueta mambo safi tu hajabeti

PAQUETA Pict

Muktasari:

  • Na sasa staa huyo wa kimataifa wa Brazil amewashukuru West Ham, familia na wanasheria wake baada ya kujinasua kwenye sakata hilo lililodumu miaka miwili.

LONDON, ENGLAND: KIUNGO wa West Ham United, Lucas Paqueta amefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili juu ya sakata la kubeti ambalo lilikuwa likimuweka kwenye hatari ya kufungiwa soka maisha.

Na sasa staa huyo wa kimataifa wa Brazil amewashukuru West Ham, familia na wanasheria wake baada ya kujinasua kwenye sakata hilo lililodumu miaka miwili.

Paqueta, 27, alisema kwenye taarifa yake iliyotolewa na klabu ya West Ham: “Tangu siku ya kwanza ya uchunguzi wa sakata hilo nilishikilia msimamo wangu wa kutokuwa na hatia juu ya shutuma hizi nzito.

“Siwezi kusema sana muda huu, lakini ningependa kumshukuru Mungu na sasa nitarudi uwanjani kucheza soka nikiwa na tabasamu usoni.

“Kwa mke wangu ambaye hajawahi kunitupa mkono, kwa West Ham, mashabiki ambao siku zote wamekuwa wakinishangilia, familia yangu, marafiki wangu na wanasheria, nawashukuru sana.”

FA ilithibitisha kwamba kamati huru ya uchunguzi juu ya madai ya kubeti yaliyokuwa yakimkabili Paqueta imebaini kwamba hayakuwa na uthibitisho wa kutosha.