Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nkunku kukwamisha dili la mkali Simons

NKUNKU Pict

Muktasari:

  • Staa wa zamani wa Leipzig, Nkunku, 27, amekuwa mchezaji mwingine wa Chelsea kuwekwa mezani kama ofa kwa ajili ya kunaswa kwa huduma ya kiungo mchezeshaji wa Kidachi, Simons.

LONDON, ENGLAND: MPANGO wa Chelsea wa kutaka kumjumuisha Christopher Nkunku kwenye dili la kumsajili Xavi Simons wa RB Leipzig linaripotiwa kufeli.

Staa wa zamani wa Leipzig, Nkunku, 27, amekuwa mchezaji mwingine wa Chelsea kuwekwa mezani kama ofa kwa ajili ya kunaswa kwa huduma ya kiungo mchezeshaji wa Kidachi, Simons.

Lakini, shida inakuja sehemu moja, Mfaransa huyo hayupo tayari kurudi kwenye klabu yake hiyo ya zamani. Na kingine, Leipzig haina uwezo wa kugharimia mshahara wa sasa wa Nkunku anaolipwa huko Stamford Bridge na kwa ripoti ya kutoka Ujerumani, analipwa Pauni 17 milioni kwa mwaka.

Mfaransa wa fowadi huyo Mfaransa anaripotiwa unaweza kushushwa, lakini bado hauwezi kuingia kwenye bajeti ya Leipzig.

Mkurugenzi wa michezo wa Leipzig, Marcel Schafer yupo kwenye presha kubwa ya kuhakikisha anapunguza kwa asilimia 20 bili ya mishahara ya klabu hiyo ili kwenda sambamba na kanuni ya matumizi ili kuiruhusu timu hiyo ya Ujerumani kucheza michuano ya Ulaya msimu huu.

Kutokana na hilo, Leipzig sasa imeamua kung'ang'ania Pauni 60 milioni kwenye mauzo ya Simons. Wakala, Ali Barat, ambaye anawasimamia mastaa wa Chelsea, Moises Caicedo na Nicolas Jackson, anafanya kazi pia ya kumsimamia Simons ili kukamilisha dili lake la kwenda kukipiga kwenye Ligi Kuu England.

Carney Chukwuemeka, Renato Veiga na Tyrique George wote waliwahi kuhusishwa kwenye dili hilo la Simons ili wao waende Leipzig.

Dili za kubadilishana wachezaji kwenye soka kwa sasa kimekuwa kitu adimu kwa sababu ya sera mpya matumizi ya pesa na jinsi malipo ya pesa za usajili yanavyokokotolewa wakati usajili wa wachezaji.