Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nigeria yashika namba tatu Afcon 2025

Muktasari:

  • Kwa ushindi huo, Super Eagles imeweka rekodi ya mara ya tisa katika historia yao ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afcon.

RABAT, MOROCCO:  NIGERIA imethibitisha nafasi yake ya tatu katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Misri.

Kwa ushindi huo, Super Eagles imeweka rekodi ya mara ya tisa katika historia yao ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afcon.

Baada ya dakika 90 za mchezo ambazo hazikuwa na purukushani nyingi, Nigeria ndiyo ilionyesha nia ya kushambulia na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga. Hata hivyo, timu zote mbili hazikuweza kutumia nafasi hizo, na mchezo kuishia suluhu.

Kwa utaratibu wa mashindano, mchezo huo uliingua moja kwa moja kwenye mikwaju ya penalti  na hakukuwa na dakika 30 za ziada kufanyakuwa dakika 120. Misri ilikosea mapema kwani nyota wao wawili, Mohamed Salah na Omar Marmoush, walikosa penalti zao baada ya kipa wa Nigeria, Stanley Nwabali kuokoa zote.

Misri haikuweza kurejea, na kuiacha Nigeria ikithibitisha nafasi yake ya tatu kwenye mashindano hayo ya Afcon 2025.