Nicolas Jackson apasua ukweli Chelsea
Muktasari:
- Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal alikuwa amesaini mkataba mpya wa miaka tisa Septemba mwaka jana, hata hivyo, hivi karibuni amepoteza namba yake kikosi cha kwanza na tayari wachezaji kama Joao Pedro na Liam Delap wameshasajiliwa kuchukua nafasi yake.
LONDON, ENGLAND: STAA wa Chelsea, Nicolas Jackson amemueleza kocha wa timu hiyo, Enzo Maresca anafikiria kujiunga na timu nyingine.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal alikuwa amesaini mkataba mpya wa miaka tisa Septemba mwaka jana, hata hivyo, hivi karibuni amepoteza namba yake kikosi cha kwanza na tayari wachezaji kama Joao Pedro na Liam Delap wameshasajiliwa kuchukua nafasi yake.
Mchezaji huyo wa zamani wa Villarreal sasa amekubaliana na Chelsea ataondoka majira haya ya kiangazi.
Jackson, 24, amekuwa akifanya mazoezi peke yake na aliachwa kwenye kikosi kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Bayer Leverkusen.
Alijiunga na Chelsea Juni 2023, kisha akasaini mkataba mpya Septemba mwaka jana na unatarajiwa kumalizika mwaka 2033.
Chelsea inataka kupata fedha kutokana na mauzo ya Jackson na wanatarajia kupata walau mara mbili ya Pauni 32 milioni walizolipa kwenda Villarreal kumsajili.
Awali ilikuwa inataka hadi Pauni 80 milioni ili kumuuza lakini sasa wanadaiwa kushusha bei yake hadi kufikia Pauni 64 milioni.
Newcastle, Bayern Munich na baadhi ya klabu za Italia zinamfuatilia mshambuliaji huyo wa Senegal na hata