Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni hivi...Vini abaki, Alonso aondoke

Muktasari:

  • Mkataba wa Mbrazili huyo, 23, unatarajiwa kumalizika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2027.

MADRID, HISPANIA: SIKU chache baada ya kuibuka kwa taarifa Vinicius Jr yupo tayari kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Real Madrid, ripoti mpya zimefichua staa huyo amegoma kusaini na amewaambia mabosi wa timu hiyo anataka Xabi Alonso aondoke ndiyo amwage wino la sivyo ataondoka yeye.

Mkataba wa Mbrazili huyo, 23, unatarajiwa kumalizika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2027.

Inadaiwa Vinicius Jr, hana uhusiano mzuri na kocha wake na suala hilo limesababisha mazungumzo ya mkataba mpya kusimama.

Inaelezwa kocha Alonso, 43, amekuwa hana imani sana na Vinicius na alipanga hadi kumweka benchi winga huyo kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia la klabu dhidi ya Paris Saint-Germain Julai mwaka huu.

Hata hivyo, jeraha la Trent Alexander-Arnold lilimfanya abadili mpango na Vinicius akaanza mchezo huo kama winga wa kulia.

Inadaiwa uamuzi huo ulimkasirisha sana Vinicius aliyemaliza nafasi ya pili katika tuzo za Ballon d’Or mwaka 2024.

Katika mazungumzo ya awali, Vinicius Jr ambaye kwa sasa  analipwa Pauni 15.8 milioni kwa mwaka baada ya kodi alipewa ofa ya mshahara wa Pauni 17.5 milioni lakiniyeye akataka alipwe Pauni 26 milioni ambacho ni sawa na kile ambacho Cristiano Ronaldo alikuwa akilipwa akiwa na Madrid.

Vinicius Jr amecheza kila mechi ya LaLiga na Ligi ya Mabingwa msimu huu na hata alipewa unahodha kwenye mechi dhidi ya Kairat Almaty Septemba mwaka huu.

Lakini katika mechi zote alizocheza, alimaliza dakika 90 katika mechi tano tu na zilizobakia zote alitolewa kabla ya kuisha.

Mshindi huyo mara mbili wa Ligi ya Mabingwa alizua utata hivi karibuni baada ya kutoa kauli ya kuonyesha kuchukizwa kwa kufanyiwa mabadiliko dhidi ya Barcelona wakati Madrid inaongoza 2-1.

Akiwa anatoka uwanjani, Vinicius alisikika akisema:"Kila mara mimi, naondoka kwenye hii timu, ni bora niondoke, naondoka."

Hata hivyo, baada ya mechi kumalizika, alitoa tamko la kuomba radhi lakini hakumtaja kocha wake katika tamko hilo.

Vinicius Jr pia amevutia anatajwa kuwa huenda akatimkia Saudi Arabia ambako Al-Ahli inahitaji saini yake na ipo tayari kufanya kufuru ya pesa ili kumpata.

Real Madrid ilitoka sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Elche wikiendi iliyopita ikisawazisha dakika za mwisho kupitia kwa Jude Bellingham na kujikita zaidi kileleni kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya wapinzani wao wa karibu Barcelona.

Leo, Jumatano watakuwa na kibarua huko Ugiriki ambapo watacheza dhidi ya Olympiacos kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuvaana na Girona Jumapili jioni, wikiendi hii.