Neymar Brazil ndio basi

Monday June 20 2022
Neymar PIC

SAO PAOLO, BRAZIL. NYOTA wa Real Madrid na timu ya taifa Brazil,  Rodrygo ametoboa siri kuwa Neyma, anajiandaa kuachana na soka la Kimataifa, baada ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyka Qatar, Novemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa fowadi huyo, Neymar amekubali kukabidhi yake,  jezi yake yenye namba 10 mgongoni, aliyokuwa akiivaa kwa muda mrefu tangu alipoanza kuichezea Brazil.
Neymar ni mfungaji wa pili wa muda wote wa taifa hilo, anajiandaa kucheza michuano yake mwisho, kabla ya kustaafu soka la Kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoiti Neymar amewaambia baadhi ya wachezaji wezake akiwemo Rodrygo, kuwa ataikabidhi jezi yake yenye namba 10 mgongoni ambayo iliwahi kuvaliwa na wakongwe kama Pelé, Ronaldinho na Kaká.
Akizungumza kupitia kituo cha televisheni cha ESPN, Rodrygo amesema “ Neymar alinambia atanipa namba ya jezi yake, nilishangaa na kukosa maneno ya kuzungumza, nilimwambia anatakiwa kuichezea Brazil mechi nyingi zaidi, sikutaka kufahamu mengi kwani alikuwa akicheka,”
Nyota huyo anayekipiga Paris Saint Germain, alianza kuichezea Brazil tangu alipokuwa na miaka 18, mwka 2010, Neymar alipachika bao lake la kwanza Kimataifa dhidi ya Marekani ndani ya dakika 28 alizocheza.
Neymar amecheza jumla ya mechi 119 na kufunga mabao 74 katika mashindano yote aliyojumuishwa kikosi, aidha nyota huyo alikosa michuano ya Copa America baada ya kupata majeraha, Brazil ikibeba ubingwa mwaka 2019.

Advertisement