Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nchi za COSAFA zaomba uenyeji AFCON 2028

PEDRO Pict

Muktasari:

  • Rais wa Shirikisho la Soka la Botswana (BFA), Tariq Babitseng, amethibitisha kukamilika kwa mchakato huo na kueleza kuwa ombi hilo lilitumwa kwa wakati na kwa kufuata taratibu zote rasmi huku wakiamini watapata heshima ya kuandaa mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

Nchi za Kusini mwa Afrika (Botswana, Afrika Kusini, Namibia, na Zimbabwe) zimewasilisha ombi la pamoja la kutaka kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2028.

Hatua hii inatajwa kuwa moja ya maombi makubwa na yenye nguvu zaidi ya pamoja kuwahi kuwasilishwa mbele ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Rais wa Shirikisho la Soka la Botswana (BFA), Tariq Babitseng, amethibitisha kukamilika kwa mchakato huo na kueleza kuwa ombi hilo lilitumwa kwa wakati na kwa kufuata taratibu zote rasmi huku wakiamini watapata heshima ya kuandaa mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.

Babitseng amefafanua kuwa lengo kuu la pendekezo hilo la pamoja ni kuunganisha nguvu kati ya mataifa hayo ya Kusini mwa Afrika ili kukuza mchezo wa soka katika ukanda huo na kuimarisha miundombinu ya michezo kwa ujumla.

ARSN 01

 Ameongeza kuwa kuna uratibu wa hali ya juu kati ya mashirikisho hayo manne, ambapo baadhi ya nchi zinatarajiwa kuwa wenyeji wa mechi za hatua ya makundi, wakati Afrika Kusini ikitarajiwa kuandaa idadi kubwa ya mechi zote za mashindano hayo.

Hatua hii ni sehemu ya maono mapana ya kukuza ushirikiano wa kikanda ndani ya Baraza la vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA), hasa baada ya motisha zilizotolewa na CAF kuhimiza uandaaji wa pamoja.

Fainali zijazo za AFCON za mwaka 2027 zitafanyika Afrika Mashariki (Kenya, Uganda, na Tanzania).