Nafasi ya Arteta shakani

Nafasi ya Arteta shakani

Muktasari:

  • Arsenal imepoteza nafasi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa na kufanya fainali zote za Ulaya kuwa kwa timu za England kutokana na suluhu iliyoipata dhidi ya Villarreal, juzi usiku.

London, England. Arsenal imepoteza nafasi ya kucheza fainali ya Ligi ya Europa na kufanya fainali zote za Ulaya kuwa kwa timu za England kutokana na suluhu iliyoipata dhidi ya Villarreal, juzi usiku.

Unai Emery alishuka kwa ajili ya kuiumiza timu yake ya zamani, huku akitumia ushindi wa nyumbani wa mabao 2-1 wa wiki iliyopita kuibana Arsenal kusaka nafasi ya kucheza fainali.

Lakini licha ya kutolewa, kocha Mikel Arteta alisisitiza kuwa yeye atabaki kuwa mtu sahihi wa kuipa Arsenal mafanikio, hata kama klabu hiyo inakutana na janga la kucheza mashindano ya Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25.

Alipoulizwa kama bado anweza kuaminika kwa kuinoa Arsenal, Arteta alisema: "Nisingekuwa hapa kama siwezi hii kazi. Mtaliona hili. Si suala la kuzungumza. Ni kufanya kazi uwanjani."

Lakini licha ya maneno hayo, nyota wa zamani wa miamba hiyo, Martin Keown amezua maswali kama Arteta kutimuliwa ama kuendelea na kibarua baada ya timu hiyo kutolewa.

Kwasasa, The Gunners ipo chini zaidi ya msimamo wa Ligi Kuu England tofauti na msimu uliopita, haina taji lolote kuonyesha kama haina ubora hata wa kutosha kuwamo katika fainali za Ulaya msimu ujao.

Keown: "Bila shaka ukiangalia katika mambo yote haya na kuchambua msimu mzima, naliona kwa macho ya mbali kabisa, nachambua na kuwaachia watu waamue wenyewe.


"Tulijaribu kila kitu hadi dakika ya mwisho, nadhani katika michezo hii miwili ya nusu fainali, kilichotokea hasa katika mchezo huu wa pili, nadhani tulistahili kuibuka na ushindi.

“Lakini namba zinatuumiza katika mchezo huu. Tulikuwa na nafasi lakini hatukuzitumia. Tuligongesha nguzo mara mbili, tulikuwa na nafasi tatu za wazi, nadhani kuna shida kwa kubaki ama kuondoka kwa Arteta."