Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Bellingham acharuka mwanaye kutolea

BABA Pict

Muktasari:

  • Mambo yalizidi kupamba moto baada ya Borussia Dortmund kupata sare ya 3-3 dhidi ya St. Pauli na baba wa Jobe Bellingham, Mark, alidaiwa kuchukulia jambo hilo kwa sheria mkononi.

MUNICH, UJERUMANI: BABA wa mchezaji Jobe Bellingham ameripotiwa kumvaa bosi wa Borussia Dortmund nje ya vyumba vya kubadilishia baada ya mwanaye kutolewa wakati wa mapumziko katika moja ya mechi za timu hiyo.

Mambo yalizidi kupamba moto baada ya Borussia Dortmund kupata sare ya 3-3 dhidi ya St. Pauli na baba wa Jobe Bellingham, Mark, alidaiwa kuchukulia jambo hilo kwa sheria mkononi.

Baada ya filimbi ya mwisho, zogo kubwa liliibuka kwenye kolido za kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia baada ya sare hiyo ya Dortmund.

Jobe, ambaye alijiunga na Borussia Dortmund kwa ada ya Pauni 32 milioni akitokea Sunderland dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, alitolewa wakati wa mapumziko katika mechi ya kwanza ya timu hiyo kwenye Bundesliga msimu huu.

Jambo hilo liliifanya Dortmund kupoteza uongozi wao wa mabao 3-1 kwa kuruhusu mabao mengine mawili na hivyo kuangusha pointi kwa sare ya 3-3.

Kwa mujibu wa Sky Sports ya Ujerumani, Mark, ambaye ni mshauri wa Jobe alionekana kutofurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kutolewa wakati wa mapumziko. Na kinachoelezwa ni hakuchukizwa tu na kitendo cha mwanaye kutolewa wakati wa mapumziko bali pia timu hiyo kucheza vibaya baada ya Jobe kutoka uwanjani.

Kwenye sakata hilo, Mark Bellingham, aliyeonekana kuwa na hasira alikuwa kwenye mazungumzo mazito na mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Sebastian Kehl. Na kinachoelezwa ni Mark Bellingham alitaka kwenda moja kwa moja kwa Kovac ili kumwambia kilichomkwaza kabla ya kukutana na bosi Kehl.