Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwaka mmoja wa Robinho jela

ROBINHO Pict
ROBINHO Pict

Muktasari:

  • Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 41 alikutwa na hatia kwenye kesi ya kubaka na mahakama ya Italia mwaka 2017, lakini alianza kutumikia kifungo chake jela huko Brazil, Machi 2024.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: STAA wa zamani wa Manchester City, Robinho amekamilisha mwaka mmoja wa kutumikia kifungo chake cha miaka tisa jela.

Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 41 alikutwa na hatia kwenye kesi ya kubaka na mahakama ya Italia mwaka 2017, lakini alianza kutumikia kifungo chake jela huko Brazil, Machi 2024.

Mwanasoka huyo wa zamani alifurahia mambo matamu ya uwanja na kufanikiwa kujiunga na Real Madrid baada ya kutamba Santos. Mwaka 2008, alikamilisha uhamisho wa kujiunga na Man City katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili, aliponaswa kwa Pauni 32.5 milioni na kucheza kwa miaka miwili. Robinho baadaye alienda AC Milan kisha China, Uturuki na kwao Brazil. Ameitumikia timu ya taifa ya Brazil mara 100.

Robinho alikutwa na hatia baada ya kushiriki kwenye kundi la uhalifu lililombaka mwanamke mmoja kwenye kumbi ya starehe za usiku huko Milan mwaka 2013.

Na sasa, staa huyo akiwa gerezani huko Sao Paulo, ameripotiwa kuungana na mfungwa mwenzake, Walter Delgatti, wakipanga kuwa na biashara ya pamoja kwa kuanzisha kampuni ya kubeti.

Delgatti, ambaye amefungwa jela miaka minane na miezi mitatu alikutwa na hatia ya kufanya udukuzi kwenye ofisi ya serikali ya Brazil ya sheria.

Robinho na Delgatti wapo kwenye selo tofauti, lakini mara nyingi wamekuwa wakikutana na kuwa pamoja kwenye viwanja vilivyo kwenye gereza hilo.

Robinho, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Robson de Souza, amekuwa akitumia muda wake gerezani kufanya kazi pamoja na kujiandikisha kwenye masomo ya kozi mbalimbali, ikiwamo ya vifaa vya umeme, akitengeneza televisheni na redio.

Robinho amejiandikisha pia kwenye kundi la wanaojisomea vitabu na kusaidia kwenye utunzaji wa bustani za mbogamboga.

Kinachoripotiwa ni Robinho amekuwa akipambana kufanya kazi ili kupata nafuu ya kutolewa kwenye gereza hilo, kitu ambacho hakijafanikiwa.