Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moyes hofu tele kumkosa Grealish

Muktasari:

  • Winga huyo anayecheza kwa mkopo kwenye kikosi chao akitokea Manchester City amekuwa na kiwango bora sana tangu alipotua Everton kwenye dirisha la majira ya kiangazi msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA, David Moyes amethibitisha kuwa Jack Grealish anasumbuliwa na maumivu ya misuli ambayo yatawaacha kwenye pigo kubwa.

Winga huyo anayecheza kwa mkopo kwenye kikosi chao akitokea Manchester City amekuwa na kiwango bora sana tangu alipotua Everton kwenye dirisha la majira ya kiangazi msimu huu.

Staa huyo amefunga mabao mawili na kuasisti mara nne, lakini sasa anakabiliwa na muda mwingi wa kuwa nje ya uwanja kutokana na maumivu hayo ya misuli. Grealish alitolewa uwanjani na nafasi yake kuingia Tyler Dibling na Moyes alisema ishu ya kumkosa winga huyo ni janga kubwa kwao.

Kocha huyo wa Everton alisema: “Jack alihisi maumivu hivyo tunahitaji kuwaangalia kwa ukaribu vijana wetu.”

Kutolewa kwa Grealish kulikuwa pigo kubwa kwa Everton katika mechi hiyo ya Stamford Bridge.

Kiungo wao aliyekuwa kwenye ubora mkubwa Kiernan Dewsbury-Hall naye alitolewa uwanjani katika mechi hiyo baada ya kuhisi maumivu na kocha Moyes alisema kuwakosa wachezaji hao kulikuwa pigo kubwa kwao kwenye mechi hiyo ya Chelsea.

Aliongeza: “Lilikuwa pigo kubwa kwetu. Kuwa nyuma kwa mabao 2-0 kulikuwa mtihani mzito kwa sababu Jack alipata nafasi ya kufunga, hakufunga.”

Everton ilikumbana na kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Chelsea, mabao ya vijana wa Enzo Maresca yakifungwa na Cole Palmer na Malo Gusto. Everton sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na mechi yao ijayo kwenye ligi hiyo itakipiga na vinara Arsenal.