Mourinho apata dili lingine

Tuesday May 04 2021
mou pic

ROMA, ITALIA. UNAWEZA ukasema ni zali. ikiwa ni siku 14 tangu afungashiwe virago na mabosi wa Tottenham, AS Roma imemtangaza Jose Mourinho kuwa atachukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kwa msimu wa 2021-2.
Mreno huyo mwenye umri wa miaka 58, ameshasaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamfanya kusalia kwenye viunga hivyo hadi mwaka 2024.
Mara baada ya kuchaguliwa Mourinho alisema; "Asante kwa familia ya Friedkin (wamiliki wa Roma) kwa kunichagua mimi kuifundisha timu hii nakuwa sehemu ya mipango yao,
"Baada ya kukaa kwenye kikazo na baadhi ya viongozi wa timu hii niligundua ubora wa mawazo yao ambayo yanalenga kuifikisha Roma mbali jambo ambalo hata mimi huwa linaishi kwenye kazi zangu.
"Vilevile sapoti ya mashabiki wa Roma, imechangia sana kunifanya nikubali kuchukua kazi hii na nina shauku sana ya kuanza kuifundisha kwa msimu ujao."
Mourinho ambaye amechukua nafasi ya Paolo Foncesca, kabla ya kukubali dili hilo, kampuni ya EuroSport ilikuwa inamshawishi kumtumia kwenye michuano ya Euro 2020 kama mchambuzi.
Kwa sasa Roma inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Serie A na wiki iliyopita ilipokea kichapo cha mabao 6-2  kutoka kwa  Manchester United katika hatua ya nusu fainali ya Europa League.


Advertisement