Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwanja wa Trent kumbakiza Salah

TRENT Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao wawili wote mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini Alexander-Arnold ataachana na miamba hiyo ya Anfield na kwenda kukipiga Real Madrid msimu ujao.

LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL ipo tayari kumpa Mohamed Salah anachotaka baada ya kumtoa Trent Alexander-Arnold kwenye vitabu vyao vya hesabu kwa maana ya mishahara ya beki huyo Mwingereza, imeelezwa.

Wachezaji hao wawili wote mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini Alexander-Arnold ataachana na miamba hiyo ya Anfield na kwenda kukipiga Real Madrid msimu ujao.

Liverpool iligomea ofa ya kutoka Saudi Arabia kumhusu Mo Salah mwaka jana na sasa inapambana kuhakikisha mkali huyo anaendelea kubaki Anfield. Na sasa kinachoelezwa ni kwamba Liverpool itakuwa na jeuri ya kumpa Mo Salah anachotaka baada ya kuwa na ziada ya pesa kutokana na Alexander-Arnold kuondoka, hivyo mshahara wake hauna kazi.

Na wakala wa Mo Salah, Ramy Abbas alisema “sasa hivi mazungumzo yamepiga hatua kuliko ilivyokuwa nyuma.”

Kinachoelezwa ni kwamba kuondoka kwa Alexander-Arnold kumekuwa na faida kubwa kwenye mazungumzo ya dili jipya la Mo Salah na kwamba Liverpool sasa itakuwa na uwezo wa kufikia matakwa ya mchezaji.