Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta kuja na mbinu ya kivita

KIVITA Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo kutoka Hispania tayari amewahi kutumia mbinu nyingine zisizo za kawaida, ikiwemo kuwaalika wezi ili kuwaibia  wachezaji wake wanapokuwa wanakula chakula ili kuwafundisha umuhimu wa kuwa makini kila wakati.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amefichua yupo katika mpango wa kushirikiana na marubani wa ndege za kivita wa jeshi la Uingereza ili kubuni njia mpya ya mawasiliano kwa wachezaji wake wanapokuwa uwanjani.

Kocha huyo kutoka Hispania tayari amewahi kutumia mbinu nyingine zisizo za kawaida, ikiwemo kuwaalika wezi ili kuwaibia  wachezaji wake wanapokuwa wanakula chakula ili kuwafundisha umuhimu wa kuwa makini kila wakati.

Aidha, aliwahi pia kuwapigia wachezaji wake wimbo “You’ll Never Walk Alone” kupitia vipaza sauti wakati wa mazoezi, ili kuwatayarisha kisaikolojia kwa mazingira yenye makelele na presha kubwa ya uwanja wa Anfield kabla ya mechi yao dhidi ya Liverpool.

KIVI 01

Sasa Arteta amekuja na ujanja mwingine. Akizungumza  na rafiki yake na ambaye ni kocha mashuhuri wa mpira wa kikapu Steve Kerr, katika moja ya hafla ya  Lead Better  alisema:”Nataka kuwasiliana na marubani wa ndege jeshi la Uingereza ili kuiga  wanavyowasiliana kwa sababu wale wanapowasiliana nina uhakika hawatumii maneno 20, huwa wanaweza kusema neno moja tu, kwa sababu ukiweka maelezo mengi unakuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha, hivyo hiyo njia yao ya kuwasiliana itakuwa nzuri sana ikiwa tutaitumia uwanjani wakati wa mechi.”

Arteta aliongeza njia hiyo itapunguza kupoteza muda mwingi katika kuwasiliana kwa jambo moja, pia itawafanya wapinzani wao kutoelewana nini wanazungumza nini.

KIVI 02

Msimu huu  kocha huyu pia ameondoa sehemu ya juu ya mlango wa kuingilia uwanjani katika Uwanja wa  Emirates ili kelele za mashabiki ziwafikie wachezaji pale  wanapoingia.

Arteta pia amepeleka mbwa aina ya Labrador katika uwanja wa mazoezi ambaye hujumuika na wachezaji kila siku ya  mazoezi.