Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kinda Arsenal afariki baada ya kuumia akiwa uwanjani

Muktasari:

  • Kupitia taarifa rasmi, klabu ya Chichester imesema: “Baada ya kupata jeraha kubwa la ubongo Jumamosi iliyopita, Billy Vigar aliwekwa katika koma. 

Mshambuliaji wa Chichester City, Billy Vigar ambaye amepata mafunzo ya kisoka katika Akademi ya Arsenal, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 21 kufuatia jeraha kubwa la ubongo alilolipata katika mchezo wa Ligi ya Isthmian uliochezwa Jumamosi iliyopita dhidi ya Wingate & Finchley, mechi ambayo ilisitishwa dakika ya 13 baada ya tukio hilo.

Kupitia taarifa rasmi, klabu ya Chichester imesema: “Baada ya kupata jeraha kubwa la ubongo Jumamosi iliyopita, Billy Vigar aliwekwa katika koma. 

"Jumanne alifanyiwa upasuaji uliolenga kuongeza nafasi ya kupona. Ingawa jitihada hizo zilisaidia kwa kiasi, jeraha hilo lilikuwa kubwa mno na alifariki Alhamisi asubuhi.”

Chichester pia imesema: “Majibu ya mashabiki na wadau wa soka tangu taarifa ya awali yalionyesha ni kwa kiasi gani Billy alipendwa na kuheshimiwa ndani ya mchezo huu. 

"Familia yake imesikitishwa sana na tukio hili lililotokea wakati akiwa anafanya kile alichokipenda zaidi ambacho ni kucheza mpira wa miguu.”

Billy Vigar alijiunga na Akademi ya Arsenal Desemba 2017 akiwa na umri wa miaka 14 na alisaini mkataba hadi Julai 2022. 

Akiwa mchezaji wa Arsenal, alicheza kwa mkopo Derby County (akichezea timu ya vijana chini ya miaka 21) na Eastbourne Borough, kabla ya kujiunga na Hastings United kwa uhamisho wa bure Julai 2024. Kabla ya kuanza msimu huu, alijiunga na Chichester City.

Klabu ya Chichester pia imetangaza kuwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Lewes iliyopangwa kuchezwa Jumamosi imeahirishwa.

Derby County, miongoni mwa klabu zilizotoa rambirambi kupitia mitandao ya kijamii, imechapisha ujumbe kwenye X (zamani Twitter) ikisema: “Watu wote wa Derby County wanasikitishwa sana na kifo cha Billy Vigar. 

"Billy alitumia nusu ya pili ya msimu wa 2022/23 akiwa kwa mkopo kutoka Arsenal, akichezea timu ya vijana chini ya miaka 21. Mawazo na sala zetu ziko na familia yake na marafiki wakati huu mgumu sana.” 

Kifo cha Billy Vigar ni pigo kubwa kwa jamii ya soka, hasa kwa vijana waliokuwa wakimwangalia kama mfano wa kuigwa.