Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta awashusha presha mashabiki Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Miamba hiyo ya Emirates iliyokusanya pointi sita katika mechi tatu ilizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, dhamira yao ni kushindana kwenye mbio za ubingwa, lakini majeruhi ya wachezaji muhimu kwenye kipindi hiki cha mwanzo wa msimu, kinampa hofu kiasi Arteta.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL, hakuna matata. Ndicho unachoweza kusema baada ya Kocha Mikel Arteta kuwa na kikosi matata kabisa licha ya mastaa wake kadhaa muhimu kuwa majeruhi.

Miamba hiyo ya Emirates iliyokusanya pointi sita katika mechi tatu ilizocheza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, dhamira yao ni kushindana kwenye mbio za ubingwa, lakini majeruhi ya wachezaji muhimu kwenye kipindi hiki cha mwanzo wa msimu, kinampa hofu kiasi Arteta.

Lakini, bosi huyo Mhispaniola kwenye dirisha la usajili wa wachezaji majira ya kiangazi alitumia zaidi ya Pauni 250 milioni kunasa mastaa wapya na kitu kizuri upande wake, wakali wote waliotua huko Emirates wapo fiti kwa mapambano.

Majeruhi waliopo kwenye kikosi cha Arsenal ni wale wachezaji waliokuwapo kwenye kikosi hicho tangu msimu uliopita; Bukayo Saka, Kai Havertz na William Saliba, ambao panga pangu walikuwa wakitengeneza Kikosi cha Kwanza cha kocha huyo kwenye harakati zake za kujaribu kuipa miamba hiyo taji la kwanza la Ligi Kuu England tangu 2004.

Maumivu ya misuli bado yanamsumbua winga Saka na kumweka nje kwa wiki kadhaa, wakati matatizo ya goti ndiyo yanayomtatiza Havertz na ataendelea kuwa nje ya uwanja hadi katikati ya mwezi ujao, huku beki wa kati Saliba alipata maumivu ya kifundo cha mguu kwenye mechi ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Liverpool wikiendi iliyopita.

Kwenye mechi hiyo ya Anfield, Arteta aliwakosa pia Ben White na Christian Norgaard, lakini kwenye benchini kulikuwa na wachezaji Martin Odegaard na Leandro Trossard, ambao awali walionekana kuwa na matatizo madogo kabla ya kupata nafasi ya kucheza katika mechi hiyo.

Lakini, kitendo cha Odegaard na Trossard kucheza kwenye timu zao za taifa Norway na Ubelgiji mtawalia kimeondoa wasiwasi kwa kocha Arteta na mashabiki wa Arsenal, wakiamini sasa watakuwa na kikosi imara katika mechi zao zijazo, licha ya kwamba wataendelea kuwakosa wachezaji wao watano muhimu hadi katikati ya mwezi huu.

Jumamosi, Arsenal itakuwa na kibarua cha kumenyana na Nottingham Forest kwenye mchezo wa Ligi Kuu England na baada ya hapo itakuwa na kipute dhidi ya Athletic Bilbao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kisha itamenyana na Port Vale katika mikikimikiki ya Kombe la Ligi kabla ya kukabiliwa na mechi ngumu za lazima ushindi dhidi ya Manchester City na Newcastle United.

Kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, Arteta amenasa huduma ya straika matata kabisa baada ya kumsajili Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon ya Ureno.

Tatizo la majeruhi kwenye kikosi chake kimemfanya Arteta ashuhudie kikosi chake kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kwa misimu mitatu mfululizo.

Mastaa wengine waliosajiliwa na Arteta kwenye dirisha la mwaka huu ni Cristhian Mosquera, Piero Hincapie, Noni Madueke, Eberechi Eze na Martin Zubimendi.


MECHI ZIJAZO ZA ARSENAL

-Septemba 13 vs Nottm Forest (nyumbani)

-Septemba 16 vs Athletic Bilbao (ugenini)

-Septemba 21 vs Man City (nyumbani)

-Septemba 24 vs Port Vale (ugenini)

-Septemba 28 vs Newcastle (ugenini)

-Oktoba 1 vs Olympiacos (nyumbani)