Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgogoro Israel, Iran waua ndugu wa mshambuliaji Inter Milan

IRAN Pict

Muktasari:

  • Taremi ambaye kucheza kombe la dunia la klabu linalofanyika Marekani ilikuwa ni ndoto yake,  kwa sasa amekwama jijini Tehran baada ya safari zote za ndege kutoka jiji hilo kusimamishwa kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya Iran na Israel.

TEHRANI, IRAN: STAA wa Inter Milan na timu ya taifa ya Iran, Mehdi Taremi ameshindwa kuungana na timu yake kwa kukosa usafiri wa kwenda Marekani kutokana na mgogoro unaoendelea baina ya nchi yao na Israel.

Taremi ambaye kucheza kombe la dunia la klabu linalofanyika Marekani ilikuwa ni ndoto yake,  kwa sasa amekwama jijini Tehran baada ya safari zote za ndege kutoka jiji hilo kusimamishwa kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya Iran na Israel.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alitarajiwa kuwasili Los Angeles kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu, kwa mujibu wa ripoti kutoka Italia.

Hata hivyo, mashambulizi ya makombora dhidi ya maeneo ya kijeshi na nyuklia ya Iran yaliyofanywa na serikali ya Israel yalisababisha anga la nchi hiyo kufungwa.

Taremi alirejea nchini mwake kuchezea timu ya taifa ya Iran katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Qatar na Korea Kaskazini.

Nyota huyo wa zamani wa Porto alicheza dakika zote katika mechi zote mbili, akifunga bao katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Korea Kaskazini.

Iran inaongoza kundi lake la kufuzu, ikiwa na alama mbili zaidi ya Uzbekistan. Ilikuwa haijapoteza mechi yoyote kabla ya kupoteza mbele ya Qatar kwa bao 1-0.

Licha ya kukwama kwake inaripotiwa Inter iko kwenye mawasiliano naye.

Inter ambayo ilipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa na kumaliza ya pili katika Serie A, itacheza kwa mara ya kwanza katika Kombe la Dunia la Klabu Alfajiri ya Jumatano dhidi ya Monterrey ya Mexico.

Inter, ambayo sasa inaongozwa na kocha mpya Cristian Chivu, itakutana pia na timu ya Japan, Urawa Red Diamonds, na vigogo wa Argentina, River Plate.

Taremi amecheza mechi 43 za michuano yote akiwa na timu hiyo  ya Italia msimu huu.