Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mexico yazindua teknolojia kali ya ulinzi World Cup

ROBOTI Pict

Muktasari:

  • Wizara ya Ulinzi ya Mexico imeonyesha teknolojia mpya ya kijeshi ikiwemo mbwa-roboti, vifaa vya kuzima mawimbi ya redio, bunduki maalumu za kudhibiti droni pamoja na mifumo ya kisasa ya kukabiliana na mashambulizi ya anga.

MEXICO CITY, MEXICO: WAKATI maandalizi ya fainali za Kombe la Dunia 2026 yakiendelea, Mexico imezindua mfumo wa kisasa wa ulinzi ya roboti la mbwa watakaotumika kuhakikisha usalama wakati wa mashindano hayo.

Wizara ya Ulinzi ya Mexico imeonyesha teknolojia mpya ya kijeshi ikiwemo mbwa-roboti, vifaa vya kuzima mawimbi ya redio, bunduki maalumu za kudhibiti droni pamoja na mifumo ya kisasa ya kukabiliana na mashambulizi ya anga.

Kwa mujibu wa maofisa wa jeshi, teknolojia hiyo inalenga kuimarisha ulinzi katika maeneo ya viwanja vya michezo na sehemu za mashabiki (fan zones), ambazo zinatarajiwa kuwa na watu wengi wakati wa mashindano hayo.

Roboti la mbwa watahusika kufanya doria, kukagua maeneo hatarishi na kusaidia kazi za ulinzi kwenye sehemu ambazo ni ngumu kufikika kwa askari wa kawaida. Wakati huo huo, vifaa vya kuzima mawimbi vitatumika kudhibiti au kuangusha droni zisizoidhinishwa zinazoweza kuhatarisha usalama wa watu wengi.

Mexico ni mmoja wa wenyeji watatu pamoja na Marekani na Canada, ambapo mechi zitachezwa katika miji ya Mexico City, Guadalupe na Monterrey.

Viongozi wa nchi hiyo wamesema lengo la kuleta teknolojia hiyo ya hali ya juu ni kuhakikisha wageni, wachezaji na mashabiki kutoka duniani kote wanapata uhakika wa usalama wa kiwango cha juu wakati wote wa mashindano.