Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi ampa mzuka dereva Formula 1

Muktasari:

  • Wawili hao walikutana katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Inter Miami CF, ikiwa sehemu ya kurudisha heshima baada ya Colapinto kumpa Messi zawadi ya kofia (helmet) ya mashindano ya mwaka jana.

MIAMI, MAREKANI: Nyota wa Inter Miami CF, Lionel Messi ametimiza ndoto ya dereva chipukizi wa Formula 1, Franco Colapinto kukutana naye kabla ya mashindano ya Miami Grand Prix nchini Marekani.

Wawili hao walikutana katika kituo cha mazoezi cha klabu ya Inter Miami CF, ikiwa sehemu ya kurudisha heshima baada ya Colapinto kumpa Messi zawadi ya kofia (helmet) ya mashindano ya mwaka jana.

Colapinto ambaye ni raia wa Argentina kama Messi, aliwahi kukiri hadharani kuwa mchezaji huyo wa soka ndiye mtu aliyekuwa anatamani zaidi kukutana naye maishani. Ndoto hiyo ilitimia akiwa ameambatana na kiungo Rodrigo De Paul ambaye ni Muargentina mwenzake anayeichezea naye Inter Miami CF, ambapo walipata muda wa faragha bila presha ya vyombo vya habari.

Akizungumza baada ya tukio hilo, Colapinto alisema ulikuwa ni wakati wa kipekee sana kwake: “Ni kitu nilichokuwa nakiota maisha yangu yote. Kama ukimuuliza Muargentina yeyote, atakuambia anataka kukutana na Leo. Kwangu ilikuwa ndoto iliyotimia.”

Dereva huyo wa timu ya Alpine F1 alisisitiza kuwa kilichoufanya kukutana na Messi kuwa na thamani zaidi ni kutokuwepo kwa kamera.

Colapinto ambaye pia ni shabiki wa soka na mfuasi wa Boca Juniors, aliongeza kuwa alifurahia kupata muda wa kuzungumza na mshindi huyo wa Ballon d’Or mara nane kuhusu maisha nje ya michezo.

Kwa sasa, kijana huyo anaelekeza nguvu zake kwenye mashindano ya Formula 1 yanayoendelea, akitarajia kuwa hamasa aliyoipata kutoka kwa shujaa wake Messi itamsaidia kufanya vizuri msimu huu.