Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo hajapenda Cameroon kuchapwa na DR Congo

Muktasari:

  • Kikosi cha Indomitable Lions kilihitaji kupata ushindi kwenye mchezo wa Alhamisi iliyopita dhidi ya DR Congo ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Amerika Kaskazini mwakani.

YAOUNDE, CAMEROON: STAA wa Manchester United, Bryan Mbeumo ameonekana kuwa mwenye huzuni kubwa baada ya timu yake ya taifa ya Cameroon kupoteza fursa ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kikosi cha Indomitable Lions kilihitaji kupata ushindi kwenye mchezo wa Alhamisi iliyopita dhidi ya DR Congo ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Amerika Kaskazini mwakani.

Mbeumo alicheza mechi hiyo iliyofanyika huko Morocco, ambapo ubao wa matokeo ulikuwa unasoma 0-0 hadi dakika 91, hapo hapo Chancel Mbemba, alipomchambua kipa Andre Onana na kuipa ushindi muhimu DR Congo inayokwenda kucheza mechi nyingine ya mchujo katika mchakamchaka wao wa kusaka tiketi hiyo ya kucheza Kombe la Dunia 2026.

DR Congo sasa itakwenda kumenyana jino kwa jino na Nigeria katika mechi ya fainali na mshindi atapata tiketi ya kwenda kucheza mechi ya mchujo dhidi ya timu za mabara mengine ili kufuzu fainali hizo za Amerika.

Mbeumo alionekana kuhuzunishwa sana na kichapo hicho, ambapo alionekana akitembelea kwenye korido za uwanjani kuelekea vyumbani akiwa peke yake na alipeana mikono kwa haraka sana na benchi la ufundi. Staa huyo sasa anajiandaa kurudi zake Man United kwenda kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton itakayofanyika baada ya mapumziko ya ligi kupisha mechi za timu za taifa kupita.

Mbeumo, 26, amekuwa kwenye kiwango bora sana katika kikosi cha Man United kwa sasa, ambapo alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba kwenye Ligi Kuu England. Katika mechi nne za ligi zilizopita, amefunga mabao manne, likiwamo la kwanza dhidi ya Tottenham kwenye sare ya 2-2 kabla ya ligi kusimama kupisha mechi za kimataifa.