Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo awasha 'moto' Cameroon ikiipiga Gabon AFCON

Muktasari:

  • Licha ya Cameroon kuingia katika mechi hiyo ikiwa na misukosuko ya kiutawala baada ya David Pagou kuchukua nafasi ya Marc Brys, walianza kwa kasi kubwa na kupata mwanzo mzuri ndani ya dakika saba tu.

CAMEROON imeanza vyema kampeni ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa ushindi wa jasho wa bao 1-0 dhidi ya Gabon, huku nyota wa Manchester United, Bryan Mbeumo akiwa mhusika mkuu akifikisha jumla ya michango mitano ya mabao (mabao na asisti katika ushindi wa mechi nne za mwisho za mashindano rasmi za Indomitable Lions).

Licha ya Cameroon kuingia katika mechi hiyo ikiwa na misukosuko ya kiutawala baada ya David Pagou kuchukua nafasi ya Marc Brys, walianza kwa kasi kubwa na kupata mwanzo mzuri ndani ya dakika saba tu.

Jina lililozoeleka liliibuka tena kuwa muhimu, pale Mbeumo alipodhibiti mpira mrefu kutoka kwa beki Samuel Kotto na kumpasia Karl Etta Eyong aliyepiga shuti kali lililomshinda kipa Loyce Mbaba.

Cameroon iliendelea kuisukuma Gabon na Danny Namaso alipata nafasi, lakini akapiga mpira nje baada ya kupokea pasi ya Junior Tchamadeu kutoka upande wa kulia.

Baadaye kocha wa Gabon, Thierry Mouyouma alifanya mabadiliko ya kushangaza ya mapema katika dakika ya 32 kwa kumuingiza Pierre-Emerick Aubameyang na Mario Lemina.

Uwepo wa nyota huyo wa zamani wa Arsenal ulionekana kuipa Gabon ari mpya, huku Denis Bouanga akiona shuti lake likizuiwa katika muda wa nyongeza wa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa juhudi nyingi kutoka pande zote na ufundi wa Mbeumo ulikaribia kuzaa matunda alipompasia Tchamadeu aliyekuwa anakimbia kwa kasi, lakini mchezaji huyo wa Stoke City alipiga shuti baya lililotoka nje.

Katika mechi hiyo, Mbeumo alionekana kuwa mzigo mkubwa kwa safu ya ulinzi ya Gabon na dakika ya 55 alikaribia kuongeza bao la pili baada ya kuwapita mabeki wawili na kupiga shuti kali lililomlazimisha Mbaba kuokoa.

Ingawa Gabon iliyo na rekodi tamu ya kufunga mabao matano ya awali baada ya mapumziko, ilizidi kuonekana kwamba ingehitaji miujiza ya kipekee ili kupata sare mbele ya Cameroon kwa jinsi ilivyobanwa kwa muda mrefu.

Aubameyang ndiye aliyekuwa tishio kubwa zaidi na alikaribia kutumia makosa karibu na eneo la hatari, lakini alijikanganya chini ya presha katika wakati muhimu.

Ingawa Gabon inaonekana kama timu dhaifu katika Kundi F hilo halikuonekana wazi kwenye mechi hiyo.

Licha ya kupoteza mechi ya ufunguzi ya AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 Gabon, ina kila sababu ya kujipanga kwa mechi ya pili dhidi ya Msumbiji itakayowalazimisha washinde ili kuweka hai tumaini la kusonga mbele.

Kwa upande wa Cameroon, mechi yao ijayo dhidi ya Ivory Coast huenda ikawa muhimu sana katika mbio za kuongoza kundi.