Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe amshutumu Arbeloa hadharani

KYLIAN Pict

Muktasari:

  • Wiki hii, Mbappe alianzishiwa benchi na kocha Alvaro Arbeloa katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania (LaLiga) dhidi ya Real Oviedo, kitendo ambacho kumbe hakukipenda licha ya kwamba bado hajawa fiti vya kutosha tangu alipoumia mazoezini kabla ya mechi dhidi ya Barcelona.

MADRID, HISPANIA: WAKATI mashabiki wa soka wa Ufaransa wakitathmini kikosi cha timu ya taifa lao (The Blues), nahodha wa taifa hilo, Kylian Mbappe ameaendeleza kile kinachoonekana kuwa hali ya mambo ndani ya Real Madrid si shwari.

Wiki hii, Mbappe alianzishiwa benchi na kocha Alvaro Arbeloa katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania (LaLiga) dhidi ya Real Oviedo, kitendo ambacho kumbe hakukipenda licha ya kwamba bado hajawa fiti vya kutosha tangu alipoumia mazoezini kabla ya mechi dhidi ya Barcelona.

Na jana, nyota huyo alifyatua kombora mtandaoni akimshutumu Arbeloa kwa kumuweka benchi wakati akiwa fiti kucheza, huku akisisitiza kwamba katika siku za karibuni amekuwa mshambuliaji wa nne katika vipaumbele vya kocha huyo.

PAZ 01

Katika posti yake kwenye akaunti yake ya X, Mbappe alidai haelewi kwa nini aliachwa benchi dhidi ya Real Oviedo na hata alipozungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo alitoa kauli nzito kuhusu nafasi yake ndani ya timu.

“Niko sawa. Nina afya kwa asilimia 100. Sikuanza leo kwa sababu kocha aliniambia kwamba kwake mimi ni mshambuliaji wa nne kwenye timu. Nyuma ya Mastantuono, Vini na Gonzalo. Nilikubali hilo na nikacheza dakika nilizopewa. Nilicheza vizuri, nilitoa asisti kwa Jude. Timu ilicheza vizuri na tukashinda... Nilikuwa tayari kuanza kama mchezaji wa kikosi cha kwanza, lakini huo ni uamuzi wake. Siwezi kumkasirikia kocha. Lazima kila wakati uheshimu maoni ya kocha.”

Mbappe aliingia uwanjani dakika ya 69 kumalizia mchezo akichukua nafasi ya Gonzalo Garcia aliyefunga bao la kwanza na la ushindi la mchezo huo. Na mara tu Mbappe alipoingia uwanjani, mashabiki walianza kumzomea.

PAZ 02

Hii inakuja baada ya Mbappe kuukosa mchezo mgumu wa El Clasico ambao Madrid walipoteza dhidi ya Barcelona, matokeo yaliyowafanya Blaugrana kusherehekea ubingwa wa La Liga.

Akijibu shutuma za Mbappe, Arbeloa alidai alitaka tu kujaribu kikosi kipya na kuwapa nafasi zaidi wachezaji wengine kwa kuwa msimu wa La Liga uko karibu kumalizika.