Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mataji ya Arteta yamshangaza shabiki

Muktasari:

  • Kocha Arteta ameibadili Arsenal na kuwa timu ya kushindania mataji tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Unai Emery, Desemba 2019.

LONDON, ENGLAND: SHABIKI mashuhuri wa Arsenal, Piers Morgan ameshangazwa na utetezi wa kocha Mikel Arteta juu ya mataji aliyobeba kwenye timu hiyo.

Kocha Arteta ameibadili Arsenal na kuwa timu ya kushindania mataji tangu alipochukua mikoba ya kuinoa timu hiyo kutoka kwa Unai Emery, Desemba 2019.

Miamba hiyo ya Emirates, tangu ilipokuwa chini ya Arteta taji kubwa pekee walilobeba ni moja, Kombe la FA katika msimu wa 2019-20.

Lakini, kocha huyo Mhispaniola alisema tena kwa msisitizo kwamba yeye ni mshindi wa mataji matatu.

Wakati alipoambiwa kwamba yeye ni mshindi wa taji moja tu, Arteta, 42, alijibu: “Na Ngao ya Jamii pia, mara mbili, siyo? Hivyo ni matatu.”

Majibu hayo ya Arteta yamemwibua shabiki mnazi wa Arsenal, Morgan, ambaye aliandika kwenye X: “Oh hapana… tafadhali niambieni siyo Arteta aliyesema.” Na hapo wafuasi wa Morgan kwenye mtandao huo, walijibu haraka, mmoja akisema: “Ndiyo, ni yeye.”

Mwingine alisema: “Hakudanganya, sivyo?”

Na shabiki wa tatu alisema: “Huo ndiyo mtazamo wake kwenye mafanikio.”

Shabiki mwingine aliweka emoji za kucheza na kusema: “Hiyo ni akili ya klabu ndogo.”

Kuna shabiki alisema: “Arteta ni (Erik) Ten Hag mpya. Isipokuwa Ten Hag ameshinda mataji mawili ya kweli ndani ya muda mchache.”

Arteta usiku wa jana Jumatano alitarajia kuiongoza Arsenal kwenye robo fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Crystal Palace.