Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Chelsea kuipa pesa familia ya Jota

MASTA 05

Muktasari:

  • Kikosi hicho cha The Blues chenye mastaa 24 waliocheza kwenye Kombe la Dunia la Klabu kilipokea bonasi ya Pauni 11.4 milioni kwa kushinda taji hilo.

LONDON, ENGLAND: MASTAA wa Chelsea watachangia sehemu ya bonasi zao watakazolipwa baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia la Klabu kwa familia ya mchezaji Diogo Jota, ambaye alifariki dunia akiwa na miaka 28.

Kikosi hicho cha The Blues chenye mastaa 24 waliocheza kwenye Kombe la Dunia la Klabu kilipokea bonasi ya Pauni 11.4 milioni kwa kushinda taji hilo.

Lakini, katika kuonyesha uungwana mkubwa, mastaa hao wa Chelsea wameamua kuchangia bonasi hiyo ili kumpa mjane wa Jota na staa huyo wa Liverpool alifariki dunia kwenye ajali ya gari akiwa na mdogo wake, Andre Silva.

Jota ameacha mke, mrembo Rute na watoto watatu. Kwa pamoja, wachezaji hao wa Chelsea wamekubaliana kufanya tukio hilo la kibinadamu la mchango wa pole.

Bado haijafahamika ni asilimia ngapi ya bonasi hiyo itatolewa kwa kila mchezaji wa Chelsea kwenda kwa familia hiyo ya Jota. Kwenye mgawo, kila mchezaji wa Chelsea alipewa Pauni 475,000 baada ya timu yao kuwa bingwa.

Lakini, bonasi yao ya jumla ilitarajia kupungua baada ya makato ya kodi na gharama za jamii kabla ya kutoa uamuzi wa kuchangia kitu kwa familia ya Jota.

Liverpool ilipanga kufanya kumbukumbu ya kipekee kwa mshambuliaji wao huyo wa Kireno mbele ya mashabiki wao huko Anfield kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth uliofanyika usiku wa jana Ijumaa.

Wachezaji wa Liverpool kwenye jezi zao kutaonekana na maandishi ya ‘Forever 20’ kwa msimu mzima kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni kumbukumbu ya staa huyo, ambaye alikuwa akivaa jezi yenye Namba 20 klabuni hapo.

Jota aliifungia Liverpool mabao 65 katika mechi 182 alizochezea miamba hiyo.

Mrembo Rute pamoja na watoto wa Jota walitarajia kuwapo uwanjani Anfield wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika usiku wa jana Ijumaa.