Marina asepa Chelsea

LONDON, ENGLAND. MKURUGENZI wa Chelsea, Marina Granovskaia ameachia ngazi wadhifa wake baada ya kudumu Stamford Bridge kwa muda wa miaka 12.
Marina anafuata nyayo za Mwenyekiti wa klabu hiyo Bruce Buck, aliyetangaza kustaafu na atakiachia kiti chake alichodumu nacho kwa muda wa 19. Aidha bosi huyo mkongwe wa muda mrefu atabaki kuwa mshauri mkuu wa klabu.
Mabadiliko hayo ya uongozi yametokana na ujio wa bilionea mpya Todd Boehly, aliyenunua klabu Chelsea baada ya kupigwa bei na Roman Abramovich.
Marina alikuwa miongoni mwa viongozi aliyefanya mambo makubwa ndani ya klabu, lakini sasa safari yake inalekea kufika ukingoni kwa mujibu wa taarifa.