Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester City kuacha mastaa kibao

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu England wamekuwa wakifanya usajili mpya tangu dirisha la Januari hadi sasa baada ya kufanya vibaya na kuachwa nyuma na Liverpool na Arsenal katika mbio za ubingwa msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City iko tayari kuwaruhusu baadhi ya nyota wake waliowahi kung’ara kuondoka katika dirisha hili la majira ya kiangazi, ikiwamo John Stones na Ilkay Gundogan, ikiwa ni muendelezo wa kocha Pep Guardiola kufanya mageuzi kwenye kikosi chake.

Mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu England wamekuwa wakifanya usajili mpya tangu dirisha la Januari hadi sasa baada ya kufanya vibaya na kuachwa nyuma na Liverpool na Arsenal katika mbio za ubingwa msimu uliopita.

Ingawa wanasaka wachezaji wapya, pia wanatarajia kuachana na baadhi ya nyota wao.

Inafahamika kuwa Guardiola anapendelea kufanya kazi na kikosi kidogo, na kwa sababu hiyo, majina makubwa yanaweza kuondoka katika dirisha hili.

Miongoni mwao, kwa mujibu wa The Athletic, ni John Stones, ambaye amekuwa mchezaji muhimu sana kwa Man City katika kipindi chao cha mafanikio.

Hata hivyo, beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 31 anatajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuuzwa msimu huu, wakati Man City ikielekea katika enzi mpya.

Gundogan, mwenye umri wa miaka 34, naye ni jina jingine kubwa linaloweza kuachwa, licha ya kwamba alirejea Etihad katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana baada ya kukaa Barcelona kwa msimu mmoja.

Kiungo huyo mkongwe anajiunga na Mateo Kovacic katika orodha ya wachezaji wanaotajwa kuwa wanaweza kuondoka, wakati klabu ikilenga kupunguza ukubwa wa kikosi.

Wachezaji wengine watatu ambao ni Nico O’Reilly, Claudio Echeverri na Oscar Bobb pia wametajwa kuwa katika hali kama hiyo kama wenzao, ingawa ripoti hiyo inaongeza kuwa Bobb huenda asiondoke Etihad kwa sasa.

Vilevile imeelezwa kuwa baadhi yao wanaweza kutolewa kwa mkopo badala ya kuuzwa moja kwa moja.

O’Reilly, mwenye umri wa miaka 20, ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango kizuri katika nusu ya pili ya msimu wa 2024-25 akiwa kama beki wa kushoto.