Man United yajiwekea rekodi mbaya

Wednesday September 15 2021
man pic

BERN, SWITZERLAND. MBONA shida. Unaambiwa kwenye mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Young Boys,  Manchester United  iliweka rekodi mbaya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 17 kupita.
Katika mchezo huo Man United  ilipiga mashuti mawili tu katika mchezo mzima na yalilenga lango la Young Boys ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Katika historia hiyo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa, hiyo ndio mechi ya kwanza katika mechi 138 zilizopita Man United kuwa na rekodi mbaya zaidi.
Man United ilifanikiwa kujipatia bao lao pekee kupitia staa wao Cristiano Ronaldo ambaye alifungwa kwa msaada mkubwa kutoka kwa Mreno mwenzake, Bruno Fernandes.
Mechi ilibadilika zaidi baada ya beki kisiki wa Man United, Aaron Wan-Bissaka  kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwani Moumi Ngamaleu alisawazisha bao dakika ya 66.
Dakika ya 95, Boys ilifunga bao la pili kupitia kwa Jordan Siebatcheu alitumia vizuri makosa ya Jesse Lingard.

Advertisement