Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yakubali hasara kwa Grealish

GRELEESH Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 100 milioni akitokea Aston Villa mwaka 2021 sio sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Marekani wiki ijayo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu chini ya kocha Pep Guardiola.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER CITY iko tayari kupata hasara ya Pauni 60 milioni kwa kumuuza Jack Grealish katika dirisha hili la majira  ya kiangazi.

Nyota huyo aliyesajiliwa kwa Pauni 100 milioni akitokea Aston Villa mwaka 2021 sio sehemu ya kikosi kitakachosafiri kwenda Marekani wiki ijayo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu chini ya kocha Pep Guardiola.

Grealish, mwenye umri wa miaka 29, ameambiwa wazi kuwa hakuna nafasi yake tena ndani ya kikosi cha Man City na klabu hiyo iko tayari kumuuza kwa bei ya punguzo ya takriban Pauni  40 milioni.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, tayari mipango imewekwa kuhakikisha anaondoka haraka, huku mawakala wake wakiwa kwenye harakati za kumtafutia timu  mpya.

Grealish anakuwa mchezaji wa pili ndani ya kikosi cha Guardiola kulazimika kuondoka, baada ya Kevin De Bruyne (33) kuambiwa anaweza kuondoka kama mchezaji huru mwishoni wa mwezi huu, licha ya yeye kutaka kusalia Etihad.

Mabeki Kyle Walker (35) na John Stones (31) pia wanatarajiwa kuondoka, huku Guardiola na viongozi wa Man City wakipanga kuleta damu changa ili kuimarisha kikosi chao chenye wachezaji wanaoonekana kujaa wazee.

Kiungo mshambuliaji wa AC Milan, Tijjani Reijnders anakaribia kusajiliwa kwa dau la Pauni 46.2 milioni na pia Man City imeripotiwa kutoa Pauni 30 milioni ili kumsajili nyota wa Olympique Lyon, Rayan Cherki.

Hadi sasa wameshafanikisha uhamisho wa Rayan Ait-Nouri kutoka Wolves kwa Pauni 34 milioni na atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoenda Marekani.

Grealish bado ana miaka miwili kwenye mkataba wake unaomwezesha kukunja Pauni 300,000 kwa wiki.

Hata hivyo, kutokana na umri wake na kiwango chake cha sasa, ni vigumu kupata mshahara kama huo kwenye timu nyingine.

Man City pamoja na Guardiola wanapanga kuhakikisha Grealish anaondoka kwa njia rahisi iwezekanavyo na wako tayari kumsaidia kupata timu mpya.

Timu zinazotajwa kumhitaji ni Aston Villa (timu yake ya zamani), Newcastle, Everton, West Ham, na Napoli.