Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City kuingilia dili la Liverpool kwa Marc Guehi

TETESI Pict

Muktasari:

  • Guehi ambaye  mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu alikuwa karibu kutua Liverpool katika dirisha lililopita  la majira ya kiangazi lakini dili lilifeli katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili.

MANCHESTER City ipo tayari kuingia vitani na Liverpool ili kuipata saini ya beki wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25.

Guehi ambaye  mkataba wake unaisha mwisho wa msimu huu alikuwa karibu kutua Liverpool katika dirisha lililopita  la majira ya kiangazi lakini dili lilifeli katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili.

Staa huyu amekuwa miongoni mwa mabeki bora wa EPL kwa misimu kadhaa na Man City inaangalia uwezekano wa kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Awali baada ya kushindwa kumsaili katika dirisha lililopita, ilielezwa Liverpool inajiandaa kumsajili Januari ambapo timu kubwa nyingine pia zilitajwa kutaka kutuma ofa kwa wakati huo lakini  baadae Liverpool ikasitisha mpango na kueleza kuwa itasubiri hadi mwisho wa msimu atakapokuwa huru.

Liverpool ilidai kwamba tetesi zinazodai kwamba Guehi anahitajika na timu nyingine kubwa kuelekea Januari sio za kweli na zimewasilishwa ili kuwapa presha wao wamsajili beki huyo Januari.

Palace italazimika kumuuza stas huyu Januari kwa sababu akikaa hadi mwisho wa msimu ataondoka bure kwa kuwa mkataba wake unamalizika wakati huo.

Man City haijawa na mwenendo mzuri kuanzia msimu uliopita na huu, inahitaji huduma ya Guehi ili kuboresha safu yao ya ulinzi.


Erling Haaland

Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta, ameweka wazi kuwa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland mwenye miaka 25, ni miongoni mwa ndoto zake.

Haaland ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2034, mara kadhaa amekuwa akihusishwa na timu hii ingawa kwa sasa ni ngumu kutokana na kiasi cha pesa kinachohitajika ili kuvunja mkataba wake kuwa kikubwa wakati uchumi wa Barca ukizidi kuwa mbaya siku hadi siku.


Almugera Kabar

KLABU ya Brentford ya Ligi Kuu England imeonyesha nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Borussia Dortmund, Almugera Kabar,  mwenye umri wa miaka 19.

Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani  ni miongoni mwa vijana waliopandishwa kutoka akademi ya Dortmund na amewahi kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani kwa vijana wenye umri chini ya  miaka 19.

Anaweza kucheza nafasi za beki wa kulia na kushoto na sehemu ya ubora wake ni kupandisha mashambulizi.


Jarrad Branthwaite

EVERTON imepania kutomwachia mshambuliaji wao Jarrad Branthwaite 23, katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Staa huyu alisani mkataba mpya wa miaka mitano Julai mwaka huu baada ya tetesi za muda mrefu zilizokuwa zikitaja kwamba anaweza kutua Manchester United au Tottenham, katika dirisha lililopita.

Everton inataka kujengea kikosi chao kicheze  kumzunguka yeye.


Jorthy Mokio

MASKAUTI wa Arsenal, Chelsea, Manchester United, Barcelona na Real Madrid wote wapo Uholanzi kumfuatilia kiungo wa Ajax Jorthy Mokio mwenye umri wa miaka 17.

Mbeligiji, miaka 17).

Staa huyu Mbelgiji ni miongoni mwa vipaji vilivyoibuka katika Ligi Kuu Uholanzi tangu msimu uliopita.

Ajax inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 20 milioni ili kumuuza mchezaji huyo katika dirisha dogo la majira ya baridi.


 Adam Wharton

KIUNGO wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England Adam Wharton, 21, anataka kusaini Liverpool licha ya kuwindwa  na Real Madrid, Chelsea na Manchester United.

 Wharton alijiunga na Palace Januari 2024 akitokea Blackburn Rovers kwa ada ya Pauni 18 milioni na sasa Palace ipo tayari kumuuza lakini wanahitaji takribani Pauni 50 milioni ambayo pia inaweza kuongezeka ikiwa kutakuwa na uhitaji wa huduma yake kutoma timu nyingine kubwa.


Manu Kone

INTER Milan inadaiwa kuanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo wa AS Roma na timu ya taifa ya Ufaransa, Manu Kone, 24,  baada ya Roma kutangaza kuwa inahitaji kuuza wachezaji kutokana na sheria za Financial Fair Play.

Roma ilikataa ofa kutoka Inter Milan msimu uliopita, lakini sasa inajiandaa kusikiliza mapendekezo kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye ipo tayari kumuuza.

Kone amekuwa katika dara za Inter kwa muda mrefu lakini kikwazo ilikuwa ni Roma.


Ademola Lookman

JUVENTUS imeshaanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Atalanta na timu ya taifa ya Nigeria, Ademola Lookman, 27, katika dirisha dogo la majira ya baridi.

Vigogo wa Juventus wanamwangalia fundi huyu kama mbadala sahihi wa straika wa kimataifa wa Serbia Dusan Vlahovic ambaye kuna asilimia kubwa akauzwa.

Lookmani, alikuwa akitaka sana kuondoka katika dirisha lililopita lakini timu zilizomhitaji zlishindwa kufikia makubakiano ya bei na Atalanta.