Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo mawili yanayombeba Erling Haaland

Muktasari:

  • Ingawa huu si mwanzo wake bora zaidi, huko nyuma amewahi kufunga mabao 11 katika mechi saba za kwanza msimu wa 2022–23 na 10 msimu uliopita, lakini hata hivyo bado anakimbiza.

Akiwa amefunga mabao tisa katika mechi saba za kwanza za Ligi Kuu England, mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland ameanza msimu huu akiwa katika moto mkali huku mambo mawili yakitajwa kumbeba katika mbio za ufungaji bora.

Ingawa huu si mwanzo wake bora zaidi, huko nyuma amewahi kufunga mabao 11 katika mechi saba za kwanza msimu wa 2022–23 na 10 msimu uliopita, lakini hata hivyo bado anakimbiza.

Moto alioanza nao msimu huu umemfanya aongoze mbio za kuwania ufungaji bora kwa tofauti ya mabao matatu dhidi ya Antoine Semenyo wa Bournemouth anayemfuatia kwa karibu. Cha kuvutia zaidi ni kwamba hakuna hata moja kati ya mabao yake tisa yaliyotokana na penalti.

Bila shaka, majeraha yanaweza kuathiri safari yake kuelekea tuzo hiyo, lakini kuna sababu mbili kuu zinazomfanya Haaland kuwa na nafasi kubwa ya kubeba tuzo ya ufungaji bora msimu huu.

Kwanza, ni idadi ya mabao aliyofunga na ubora wa nafasi anazopata. Pili, ni mwanzo hafifu wa wapinzani wake wa kawaida kama Mohamed Salah.

Kipimo cha makadirio ya kufunga bao huonyesha wastani wa mchezaji angetarajiwa kufunga kutokana na ubora na idadi ya nafasi alizopata. Hii si takwimu ya kubuni, bali ni matokeo ya uchambuzi wa historia ya Ligi Kuu England.

Ukiangalia wachezaji wa Premier League msimu huu, Haaland anaongoza kwa nafasi bora za kufunga kuliko mchezaji mwingine yeyote. Hata kama kiwango chake cha kumalizia nafasi kingekuwa cha kawaida tu, bado angekuwa amefunga zaidi ya mara mbili ya wachezaji wengine.

Takwimu zinaonyesha Haaland amepiga mashuti 29 hadi sasa, mashuti 12 zaidi ya mchezaji mwingine yeyote. Hata hivyo, si idadi hiyo pekee ya mashuti inayovutia, bali ubora wa nafasi hizo. Mashuti yake yamekuwa na wastani wa thamani ya makadiria ya kufunga 0.27, ikimaanisha kihistoria nafasi hizo huzalisha mabao kwa asilimia 27.

Kwa mchezaji aliyepiga angalau mashuti 10, ni Enzo Fernández pekee wa Chelsea aliyepata nafasi rahisi zaidi kufunga dhidi ya West Ham na Brighton.

Haaland amepiga hatua kubwa ikilinganishwa na msimu uliopita, ambapo alikuwa na wastani wa kufunga 0.17 kwa kila shuti. Hii inaonyesha kwamba mfumo mpya wa Manchester City msimu huu unamuwezesha kupata nafasi rahisi zaidi kufunga.

Kuanza msimu kwa kasi kubwa si jambo geni kwa Haaland. Msimu uliopita, baada ya mechi saba, alikuwa amefunga mabao 10, manne zaidi ya mchezaji mwingine na sita zaidi ya Salah. Hata hivyo, mwisho wa msimu Salah ndiye aliyechukua kiatu cha dhahabu kwa mabao 29, saba zaidi ya Haaland.

Msimu huu, Haaland ameanza kwa kasi, huku Salah akiwa na nusu ya mabao aliyokuwa nayo katika kipindi hiki msimu uliopita, na idadi ndogo zaidi ya nafasi ya kufunga. Kwa kweli, huu ndio mwanzo wake wa taratibu zaidi tangu aanze kucheza Ligi Kuu England.

Si Salah pekee anayesuasua. Ukiangalia wafungaji 11 bora wa msimu uliopita, Haaland amefunga mabao sawa na jumla ya hao 10 waliobaki kwa pamoja.

Wengine kama Yoane Wissa, Cole Palmer, Jørgen Strand Larsen, Alexander Isak, Bryan Mbeumo, Chris Wood, Ollie Watkins na Matheus Cunha wameshindwa kuonyesha makali yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo majeraha, usumbufu wa usajili au timu zao kutoanza vizuri.

Kwa hali hii, Haaland anaonekana kuwa mshindi mtarajiwa wa Kiatu cha Dhahabu cha Premier League, lakini vipi kuhusu Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya kinachotolewa kwa mfungaji bora katika ligi tano bora za Ulaya?

Mbio hizo bado ni ngumu kwani Harry Kane (11) na Kylian Mbappé (9) nao wameanza vyema. Lakini kutokana na ukweli kwamba Haaland hajafunga penalti yoyote hadi sasa na bado anaongoza kwa idadi ya nafasi bora zaidi, anabaki kuwa mshindani mkuu.

Hata hivyo, Kane na Mbappé ni miongoni mwa washambuliaji bora zaidi duniani katika kutumia nafasi ndogo, jambo linalofanya pambano hili la Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya kuwa lenye ushindani mkali zaidi msimu huu.