Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mainoo ahakikishiwa maisha Man United

Muktasari:

  • Carrick alimpa Mainoo nafasi yake ya kuanza mchezo kwenye Ligi Kuu England msimu huu wakati wa ushindi mkubwa wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kwenye dabi ya Manchester iliyofanyika Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: MICHAEL Carrick amesema Manchester United inahitaji wachezaji kama Kobbie Mainoo, akiwataja kuwa ni “msingi wa klabu”.

Carrick alimpa Mainoo nafasi yake ya kuanza mchezo kwenye Ligi Kuu England msimu huu wakati wa ushindi mkubwa wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester City kwenye dabi ya Manchester iliyofanyika Old Trafford.

Mainoo anatarajiwa kufungua upya mazungumzo ya mkataba mpya na Man United baada ya majadiliano kusimama mapema mwaka 2025, kutokana na wasiwasi wa majeraha na kukosa muda wa kucheza msimu uliopita.

Akizungumza na vyombo vya habari Ijumaa, Carrick, 44 alisema: “Nimefurahia sana kufanya kazi na Kobbie. Ninamfahamu tangu alipokuwa mdogo, nadhani nilianza kufanya kazi naye kidogo alipokuwa na umri wa miaka 13 au 14 nilipokuwa nikifanya kozi zangu za ukocha. Klabu hii inahitaji vijana wanaopanda ngazi na kuwa msingi, ili waelewe maana halisi ya klabu. Hili ni jambo tunalopaswa kulizingatia na kuendelea kujenga juu yake.

“Kobbie ni mfano bora, kupanda kwake kwa haraka na kucheza michezo mikubwa akiwa na umri mdogo kiasi hicho kunaonyesha ubora mkubwa wa tabia na uwezo wa kubeba presha. Sehemu ya taaluma ya mchezaji ni kupitia kupanda na kushuka, lakini tuliona wiki iliyopita kile anachoweza kufanya. Ni mtulivu kiasi, lakini unaweza kuona kupitia uchezaji wake alivyokuwa anajifurahia. Kumuona hivyo ilikuwa jambo zuri sana.”

SunSport ilifichua kwa kipekee kuwa Carrick alizungumza na Mainoo baada ya kuteuliwa kama kocha wa muda, akimwambia kuwa atakuwa sehemu muhimu ya mipango yake hadi mwisho wa msimu. Mainoo alikuwa bora sana kwenye dabi, akicheza dakika 90 kwa mara ya kwanza msimu huu tangu Man United walipotolewa vibaya kwenye Kombe la Carabao na timu ya daraja la chini Grimsby.

Mhitimu huyo wa akademi mwenye umri wa miaka 20 aliporomoshwa kwenye mpangilio wa kikosi chini ya aliyekuwa kocha mkuu, Ruben Amorim katika kipindi chake cha miezi 14 madarakani. Kuondoka kwa Casemiro mwishoni mwa mkataba wake msimu wa joto kutatoa nafasi ya kifedha kwa Man United kufanya usajili mkubwa wa kiungo cha kati ili kuja kucheza na Mainoo. Viungo wanaotajwa ni Elliot Anderson, Adam Wharton, Alex Scott na Carlos Baleba.