Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahrez aanza kwa moto Afcon 2025

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Algeria, ambao ni mabingwa wa Afcon 2019, walikuwa na wakati mzuri katika mechi hiyo na hivyo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

RABAT, MOROCCO: MABAO mawili ya Riyad Mahrez yalitosha kwa Algeria kupata ushindi wa kibabe dhidi ya Sudan iliyocheza na wachezaji 10 uwanjani katika mechi yao ya kwanza ya Kundi E la mashindano ya Afcon 2025 iliyofanyika Rabat.

Algeria, ambao ni mabingwa wa Afcon 2019, walikuwa na wakati mzuri katika mechi hiyo na hivyo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Winga huyo wa zamani wa Manchester City, Mahrez aliipa timu yake mwanzo mzuri baada ya kufunga kwa guu la kushoto kutoka kwenye umbali wa mita 12 baada ya pasi ya kisigino ya Hicham Boudaoui.

Yaser Awad Boshara alimpa majaribio mara mbili kipa wa Algeria, Luca Zidane, lakini Sudan ilikosa maajabu baada ya Salah Adel kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano dakika sita kabla ya filimbi ya mapumziko.

Mahrez, 34, aliongeza bao la pili katika kipindi cha pili alipofunga kwa utulivu mkubwa ndani ya boksi baada ya pasi safi ya kupenyeza ya Mohamed Amoura.

Straika wa Wolfsburg, Amoura nusura aongeza bao la tatu, kabla ya Ibrahim Maza hajaitendea haki kazi nzuri ya Baghdad Bounedjah nje ya boksi la penalti na kufunga bao la tatu dakika tano kabla ya filimbi ya mwisho na hivyo kuifanya Algeria kufunga bao la 100 kwenye Afcon.

Kisha kipa wa Sudan, Monged Elneel alifanya sevu mbili kwenye dakika za majeruhi kumgombea mtokea benchini Adil Boulbina.

Algeria sasa inaongoza Kundi E kwa tofauti ya mabao juu ya Burkina Faso, ambayo iliichapa Equatorial Guinea 2-1 katika mechi ya mapema.