Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Macho yote kwa Sesko, Gyokeres

MACHO Pict

Muktasari:

  • Timu hizo zote mbili zimefanya usajili mkubwa dirisha hili, ikiwamo mastraika wawili matata kabisa, ambao watakuwa vivutio vya mashabiki wengi wakati wa mchezo huo utakaofanyika Old Trafford, Jumapili.

MANCHESTER, ENGLAND: NI balaa. Manchester United na Arsenal zitapigana vikumbo wikiendi hii katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England.

Timu hizo zote mbili zimefanya usajili mkubwa dirisha hili, ikiwamo mastraika wawili matata kabisa, ambao watakuwa vivutio vya mashabiki wengi wakati wa mchezo huo utakaofanyika Old Trafford, Jumapili.

Macho ya wengi yatakuwa kwa mastraika Benjamin Sesko wa Man United na Viktor Gyokeres wa Arsenal na kila mmoja atakuwa jukumu la kuibeba timu yake katika mechi ya kwanza ya ligi. Sesko alinaswa kwa Pauni 74 milioni na kwenda kuungana na safu mpya ya ushambuliaji huko Old Trafford sambamba na Bryan Mbeumo na Matheus Cunha.

Wakati huo, Arsenal nayo ikitarajia kuwa na safu matata kabisa ya ushambuliaji itakayoundwa na Gyokeres, Bukayo Saka na Noni Madueke. Patachimbika.

Nani atakuwa staa wa mchezo, Sesko au Gyokeres? Ni suala la kungoja.

Mechi hiyo itamshuhudia kocha wa Man United, Ruben Amorim akikutana na straika wake wa zamani, Gyokeres, ambaye aliwahi kumnoa huko Sporting Lisbon, lakini Mikel Arteta wa Arsenal naye atakabiliana na mshambuliaji ambaye alijaribu kumsajili kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, Sesko.

Amorim na Arteta wanatarajia kuonyeshana ufundi mwingi, huku vita kali inatarajia kuwa kwenye eneo la kati ya uwanja kwa viungo kuonyeshana ubabe.

Eneo jingine litakalokuwa kwenye mtihani mzito ni la mabeki wa pande zote mbili, kutokana na safu za ushambuliaji za timu hizo mbili kuonekana kuwa balaa. Itakuwaje? Ukiweka kando kipute hicho cha Old Trafford, mcha -kamchaka wa Ligi Kuu England unaendelea na Jumamosi hii na Aston Villa itakipiga na Newcastle United, Brighton ikicheza na Fulham, Sunderland na West Ham United, Tottenham Hotspur itacheza na Burnley na Wolves itaonyeshana ubabe na Manchester City.

Kwa Jumapili, mechi nyingine mbili zitakazopigwa ni pamoja na Chelsea itakayokuwa Stamford Bridge kucheza na Crystal Palace na Nottingham Forest itakipiga na Brentford. Jumatatu kutakuwa na mechi moja tu na kasheshe litakuwa baina ya Leeds United itakayomaliza ubishi na Everton.